Pata taarifa kuu
CANADA-USALAMA

Watu 10 wauawa kwa kugongwa na gari Toronto, Canada

Watu kumi wamepoteza maisha baada ya mwanaume mmoja aliyekuwa akiendesha gari kugonga umati wa watu katika jiji la Toronto nchini Canada,tukio ambalo polisi imeliita shambulizi la makusudi.

Polisi inachunguza gari la mizigo lililogonga watu kadhaa Jumatatu, Aprili 23 huko Toronto, na kuua watu kumi na kuwajeruhi wengine kumi na sita.
Polisi inachunguza gari la mizigo lililogonga watu kadhaa Jumatatu, Aprili 23 huko Toronto, na kuua watu kumi na kuwajeruhi wengine kumi na sita. Cole Burston/Getty Images/AFP
Matangazo ya kibiashara

Kisa hicho kilitokea jumatatu mchana katika eneo lenye umbali wa kilomita 16 kutoka ukumbi wa mkutano wa mawaziri wa mataifa makubwa kiviwanda G7.

Maafisa wanasema tukio hilo halihusiani na mkutano huo.

MKUU wa polisi katika jiji hilo Mark Saunders amethibitisha idadi ya vifo na kusema shambulizi hilo lililkuwa la makusudi.

Kumekuwa na matukio ya magari makubwa kutumiwa na magaidi kusababisha vifo katika maeneo yenye mikusanyiko,baada ya mamlaka za usalama kudhibiti njia za magaidi hao zilizooeleka.

Waziri wa usalama wa Canada Ralph Goodale amewaambia waandishi wa habari kwamba ni mapema kusema tukio hilo ni la kigaidi.

"Kuna ushirikiano wa kutosha kwa Polisi,katika kuchunguza jambo hilo,na tutatoa majibu ya hili kwa umma.Lakini kwa sasa hakuna taarifa zozote kwangu kuhusiana na chanzo ama lengo la tukio hili.'' Ralph Goodale

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.