Pata taarifa kuu
MAREKANI-KOREA KASKAZINI-USHIRIKIANO

Trump atishia kujiondoa kwenye mazungumzo na Kim kama hakuna maendeleo

Rais wa Marekani Donald Trump amesema, iwapo mazungumzo kati yake na kiongozi wa Korea Kaskazini, hayataonekana kuzaa matunda atajiondoa.

Rais wa Marekani Donald Trump  atarajia kukutana ana kwa ana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un..
Rais wa Marekani Donald Trump atarajia kukutana ana kwa ana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un.. REUTERS/Lucas Jackson
Matangazo ya kibiashara

Aidha, amesema kumekuwa na shinikizo za kutosha kuhakikisha kuwa Korea Kaskazini inaachana na mradi wake wa nyuklia.

Trump pia amethibitisha kuwa aliyakuwa Mkurugenzi wa CIA, Mike Pompeo, alikutana kwa siri na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un.

Rais Trump alisema katika mkutano wa pamoja kwamba iwapo anadhani kwamba mkutano huo hautafanikiwa basi hatoshiriki na kwamba iwapo mkutano huo umefanyika na haoni matunda yake basi atasimama na kuondoka.

Trump na Kim Jong Un wanatarajiwa kukutana ana kwa ana hivi karibuni.

Katika mkutano na Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe, Bwana Trump alisema kuwa Marekani itaendelea kupinga hatua ya kujiunga na biashara ya ushirikiano ya Trans Pacific Partnership hadi pale Japan na washirika wengine watakapoweka makubaliano ambayo Marekani haiwezi kukataa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.