Pata taarifa kuu
MAREKANI-AFYA-HAKI

Mke wa rais wa zamani wa Marekani George HW Bush aaga dunia

Barbara Bush, mke wa aliyekuwa rais wa zamani wa Marekani na mwanaharakati amefariki akiwa na umri wa miaka 92. Mama wa Taifa wa zamani nchini Marekani, Barbara Bush aliaga dunia Jumanne Aprili 17, 2018, Houston, Texas, baada ya kuugua kwa muda mrefu.

(Picha ya maktaba) Barbara Bush (katikati), mke wa rais wa zamani wa Marekani George H. W. Bush na mama wa rais mwingine wa nchi hiyo,George W. Bush, aliaaga dunia Jumanne Aprili 17 akiwa na miaka 92.
(Picha ya maktaba) Barbara Bush (katikati), mke wa rais wa zamani wa Marekani George H. W. Bush na mama wa rais mwingine wa nchi hiyo,George W. Bush, aliaaga dunia Jumanne Aprili 17 akiwa na miaka 92. REUTERS/Jason Reed
Matangazo ya kibiashara

Barbara Bush pia alikuwa mama wa taifa la Marekani baada ya kuwa mkewe rais na kisha akamzaa mwana aliyeishia kuwa rais.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari,familia hiyo imesema kuwa mama huyo ambaye amekuwa akiugua maradhi kadhaa hatari kwa maisha ya binadamu na amekata roho akiwa na umri wa miaka 92.

Mnamo Jumapili, siku mbili tu kabla ya yaliyoikuta familia, Msemaji wa familia hiyo, Jim McGrath katika taarifa alikuwa amesema: "Kwa sasa familia ya Barbara Bush inashukuru Mungu kwa kuwapa maisha na mama huyo na kwa sasa itazingatia kumfariji katika kitanda chake cha kuugua na kumwonyesha mapenzi ya kuwa wa familia moja nao."

Magonjwa ambayo amekuwa akitibiwa yanajumuisha thyroid, ugonjwa wa moyo na pia vidonda vya tumbo.

“Barbara Bush kwa wengi amekuwa ngome ya kuwa ngangari katika hali yake ya kiafya na badala ya kuihurumia, amekuwa akihurumia wengine walio katika changamoto za kimaisha,” Msemaji wa familia hiyo, Jim McGrath katika taarifa.

Jim McGrath anasema kuwa kwa sasa mama huyo amezingirwa na familia yake pana na ambayo kwa maombi wako pamoja na pia katika kumdhihirishia kuwa hayuko peke yake akiiendelea kutegemea imani yake thabiti kwa Mungu.

Barbara Bush ni wa pili kuwa mama wa taifa na kisha kuwa mama kwa rais wa taifa katika taifa hilo, kando na Abigail Adams ambaye alikuwa mkewe rais John Adams aliyekuwa rais wa pili wa Marekani na kisha akawa mama kwa rais wa sita wa taifa hilo, John Quincy Adams.

Salamu za rambirambi zimetumwa nchini Marekani kutoka maeneo tofauti duniani.

Mumewe aliye na umri wa miaka 93 ndiye rais aliyeishi kwa muda mrefu nchini Marekani.

Barbara Bush mke wa rais kutoka 1989 hadi 1993 afya yake imekuwa ikiyumba kwa muda sasa na alikuwa amekataa kupatiwa matibabu zaidi.

Awali alikuwa ameamua kumuachia Mungu akisema hahitaji kwenda hospitalini kutafuta matibabu baada ya kuchoka kutanga na njia.

Familia ya aliyekuwa Rais, George Bush, juzi ilitoa taarifa ikisema kuwa mamake, Barbara Pierce Bush hangesaka matibabu tena bali atangoja hatima ya Mungu atakavyoamua; na sasa ameshafariki.

Mumewe aliye na umri wa miaka 93 ndiye rais aliyeishi kwa muda mrefu nchini Marekani.

Mtoto wao George alichaguliwa 2000 na kukaa madarakani kwa mihula miwili kama rais wa 43 wa Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.