Mkurugenzi wa zamani wa FBI, ambaye Trump alimfukuza mnamo mwezi Mei 2017, amerejelea habari za kisiasa za Marekani tangu kuchapishwa juma lililopita, maelezo mafupi ya kitabu chake kitakachotolewa siku ya Jumanne wiki hii.
Katika kitabu hicho "A Higher Loyalty, Truth, Lies and Leadership" amemfananisha rais wa Marekani na kiongozi wa kundi kutoka jamii ya mafia.
Katika mahojiano ya muda mrefu na ABC yaliyorushwa Jumapili usiku, Mkurugenzi wa zamani wa FBI anasema kwamba Trump "hafai kimaadili" kutekeleza majukumu yake ya urais na amefanya "uharibifu mkubwa" kwa viwango vya taasisi za Marekani .
"Kimaadili hafai"
"Sijasema kuwa ana tatizo la akili kwa kuwa rais, ninasema hafai kimaadili kuwa rais," Bwana Comey amesema.