Pata taarifa kuu
MAREKANI-MEXICO-USALAMA

Trump kutuma askari kwenye mpaka na Mexico

Rais wa Marekani Donald Trump amesema yuko tayari kutuma askari kulinda mpaka wa kusini mwa Marekani, unaohatarishwa na viongozi wenye uchu wa madaraka wa Mexico. Rais Trump amekosoa vikali maamuzi ya mtangulizi wake, Barack Obama.

Rais wa Marekani Donald Trump anatoa maoni juu ya Mpango wa Miundombinu wa Ndani katika Kituo cha Mafunzo cha Richfield Training Site, Ohio, Marekani, Machi 29, 2018.
Rais wa Marekani Donald Trump anatoa maoni juu ya Mpango wa Miundombinu wa Ndani katika Kituo cha Mafunzo cha Richfield Training Site, Ohio, Marekani, Machi 29, 2018. REUTERS/Yuri Gripas
Matangazo ya kibiashara

"Mpaka tuwe na ukuta na usalama wa kutosha, tutalinda mpaka wetu kwa jeshi letu, ni hatua kubwa," Trump alisema baada ya mkutano na viongozi watatu wa majimbo ya Baltic katika ikulu ya White House siku ya Jumanne Aprili 3.

Wakati huo huo balozi wa Mexico nchini Marekani, Geronimo Gutiérrez, amesema kuwa aliiomba Marekani kutoa maelezo zaidi kuhusu hatua hiyo. "Serikali ya Mexico itaamua kuhusu jibu lake kulingana na ufafanuzi huu na italinda daima uhuru wetu na maslahi ya taifa," waziri wa Mambo ya Nje wa Mexico, Luis Videgaray, ameongeza kwenye Twitter.

Ikulu ya White House ilisema Jumanne jioni kuwa Donald Trump "alifahamishwa wiki iliyopita na viongozi wakuu wa utawala kuhusu idadi kubwa ya wahamiaji haramu wanaoingia nchini Marekani, madawa ya kulevya na makundi ya wahalifu yanayotokea Amerika ya Kati." Katika mkutano huo, ambapo walihudhuria mawaziri wake wa ulinzi, usalama na sheria, "aliagiza kuepo na mkakati muhimu kutoka kwa utawala wake ili kukabiliana na tishio hili na kulinda usalama wa Amerika."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.