Pata taarifa kuu
BRAZIL-RUSHWA-HAKI

Hatima ya Lula kujulikana Jumatano

Mahakama Kuu ya Brazil (STF) inatarajia kutoa uamuzi wake leo Jumatano kama Lula atakwenda jela katika siku zijazo au la, ikiwa imesalia miezi sita tu kabla ya uchaguzi wa urais. Katika uchaguzi huo kiongozi huyo wa mrengo wa kushoto anapewa nafasi kubwa ya kushinda.

Uhuru wa Luiz Inacio Lula da Silva mikononi mwa Mahakama Kuu Brazil.
Uhuru wa Luiz Inacio Lula da Silva mikononi mwa Mahakama Kuu Brazil. AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika Mahakama ya Rufaa, Luiz Inacio Lula da Silva alihukumiwa kifungo cha miaka 12 na mwezi mmoja kwa kosa la rushwa.

Luiz Inacio Lula da Silva, mwenye umri wa miaka 72, ana matumaini kwamba mahakama ya juu zaidi nchini humo "itakubali hoja ya kutomuweka jela" mpaka kukamilika kwa taratibu zote za kisheria.

Majaji 11 wanatarajia kutoa uamuzi, mmoja baada ya mwingine, wakati wa kura inayoonekana kukaribiana.

Polisi wameweka katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kwenye makao makuu ya mahakama Kuu (STF) ili kuepuka vurugu kati ya wafuasi na wale wanaompinga Lula da Silva ambao wamepanga kuandamana mbele ya makao makuu ya Mahakama Kuu.

Siku ya Jumanne jioni, maelfu ya wapinzani wa rais wa zamani waliingia mitaani katika mijii mikubwa ya Brazil, ikiwa ni pamoja na Sao Paulo na Rio de Janeiro.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.