Pata taarifa kuu
MAREKANI-UN

UN: Marekani yashinikiza nchi wanachama kuchangia zaidi

Balozi wa Marekani kwenye umoja wa Mataifa Nikki Haley ameziambia nchi wanachama kwenye umoja wa Mataifa kuwa zinahitajika kuongeza fedha zaidi kwaajili ya kufadhili operesheni za kulinda amani.

Balozi wa Marekani kwenye umoja wa mataifa Nikki Haley.
Balozi wa Marekani kwenye umoja wa mataifa Nikki Haley. REUTERS/Lucas Jackson
Matangazo ya kibiashara

Mchangiaji mkubwa wa operesheni za kulinda amani za umoja wa Mataifa nchi ya Marekani alitaka kupunguzwa kwa dola za Marekani milioni 600 katika bajeti yake lakini Heley sasa ameweka wazi kuwa Serikali yake inataka kupunguza zaidi mchango wake.

Haley ameziambia nchi wanachama za baraza la usalama kuwa nchi yake itaendelea kusalia kuwa mchangia mkubwa wa fedha kwenye umoja wa Mataifa lakini itapunguza asilimia 25 zaidi katika kiwango cha sasa cha asilimia 28.5.

"Nchi moja haipaswi kuachwa peke yake ichangie karibu robo tatu ua bajeti ya operesheni za kulinda amani, na tunatarajia kuona nchi nyingi zaidi zikichangia kwa usawa."

"Kuelekea mbele Marekani haitalipa zaidi ya asilimia 25 ya bajeti ya kulinda amani."

"Sote tunaowajibu na sote tunapaswa kuongeza nguvu."

Baada ya mjadala mkali wa nchi wanachama, nchi wanachama 193 ziliridhia kuwa bajeti ya walinda amani kwa mwaka 2017-2018 ilitengwa kuwa bilioni 6.8 huku nchi 10 zikitakiwa kulipa zaidi.

baada ya Marekani, nchi ya China ni taifa la pili linalochangia ikilipa asilimia 10.25 ya bajeti ikifuatiwa na Japan, Ujerumani, Ufaransa, Uingereza, Urusi, Italia, Canada na Uhispania.

Kiwango cha asilimia 25 cha mchango unaotolewa na Marekani kiko kwenye sheria ya Marekani tangu mwaka 1990, lakini baraza la Congress liliwahi kufanyia marekebisho sheria hiyo.

Tangu kuingia madarakani kwa Serikali ya rais Donald Trump amekuwa mgumu kutoa fedha kwa umoja wa Mataifa, akipunguza michango yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.