Pata taarifa kuu
CHINA

Rais wa China ayaonya mataifa yanayotishia ustawi wake

Rais wa China Xi Jinping ametoa hotuba kali na yakizalendo Jumanne ya wiki hii, akionya kuwa jaribio lolote la kuigawa nchi yake na kuijaribu uwezo wa kupigana, ijiandae kwa vita kuu katika kuirejesha nchi hiyo kwenye nafasi yake kidunia.

Rais wa China Xi Jinping, akihutubia mkutano mkuu wa chama chake. 20 Machi 2018
Rais wa China Xi Jinping, akihutubia mkutano mkuu wa chama chake. 20 Machi 2018 REUTERS/Damir Sagolj
Matangazo ya kibiashara

Hotuba ya Xi imehitimisha kongamano la kitaifa la chama tawala cha Kikomunist, kongamano ambalo lilimuidhinisha pia kuwa rais wa maisha na kumfanya kuwa kiongozi mwenye nguvu tangu utawala wa Mao Zedong, akipewa nafasi ya kubadili nchi hiyo katika nguvu za kijeshi na uchumi wenye nguvu.

Siku chache tu baada ya rais Donald Trump kutia saini sheria mpya kuruhusu maofisa wake kwenda nchini Taiwan, rais Xi ameonya kuwa Beijing itajilinda kwa vyovyote vile hasa katika kulinda visiwa vilivyo chini yake.

"Vitendo vyote na ujanja kujaribu kuigawa nchi vitaenda kushindwa na kulaaniwa na watu na hostoria pia," alisema Xi wakati akihutubia wajumbe zaidi ya elfu 3 waliohudhuria kikao kilichofanyika kwenye eneo la Great Hall.

Kwa upande mwingine rais Xi pia ameelezea nia ya nchi ya China kujipanua kimaendeleo kupitia miradi mbalimbali inayofadhili na kuongeza kuwa haitakuwa kitisho kwa taifa lolote.

"Ni wale tu ambao wamezoea kutishia wengine ndio watawaona wenzao kama kitisho," aliongeza rais Xi ambaye wajumbe walilipuka kwa shangwe.

Nchi ya China inasimamia mradi mkubwa wa ujenzi wa miundombinu kufufua njia ya Silk, ikipata uungwaji mkono kwa mataifa mengine kuunga mkono huku baadhi wakikosoa wakidai inalenga kuinufaisha nchi ya China peke yake.

Mpango wa rais Xi kuimarisha jeshi lake kuwa jeshi lenye nguvu kidunia pia ni suala linaloonekana kuyagusa baadhi ya mataifa kutokana na kuongeza nguvu ya kijeshi na migongano ya kikanda kuhusu visiwa vya bahari ya kusini.

Xi alitumia sehemu ya hotuba yake yote kueleza maono yake kwa taifa lenye nguvu la China akisema ni dnoto ya kuwa taifa la pili duniani lenye uchumi imara.

"Watu wa China wamekuwa wavumilivu na wakomavu, tunayo roho ya kupambana dhidi ya maadui wetu hadi mwisho," alisema rais Xi.

Hata hivyo hotuba yake oia imewakumbusha watu kuwa chama tawala cha Communist ndio kwanza kimeanza na kuendelea kujikita madarakani na kujihusisha pakubwa kwenye masuala ya nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.