Kusikiliza Pakua Podcast
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
  Uchambuzi na makala 21/01 04h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
  Uchambuzi na makala 21/01 05h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
  Uchambuzi na makala 20/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
 • Syria: Watu kumi na mmoja wauawa katika mashambulizi ya anga ya Israel (Shirika lisilo la kiserikali)
 • ELN yakiri kuhusika katika shambulio dhidi ya chuo cha polisi Bogota (taarifa)
Amerika

Rais Trump amfuta kazi Tillerson, amteua Mike Pompeo

media Rais wa Marekani Donald Trump REUTERS/Chris Keane

Rais wa Marekani Donald Trump amemfuta kazi Waziri wake wa Mambo ya nje Rex Tillerson na kumteua Mkurugenzi Mkuu wa CIA Mike Pompeo kuchukua nafasi hiyo.

“Mike Pompeo, Mkurugenzi wa CIA, atakuwa Waziri wetu mpya wa Mambo ya nje. Atafanya kazi nzuri,” Trump ameandika kupitia ukurasa wake wa Twitter.

“Asante sana Rex Tillerson kwa huduma yako,” aliongeza rais Trump.

Aidha, amesema kuwa alitofautiana na Tillerson kuhusu baadhi ya masuala hasa kuhusu mkataba wa Iran, kati ya nchi hiyo na nchi za Magharibi.

"Namtakia Tillerson kila la heri, amekuwa mtu mwema sana," alisema Trump.

Hatua hii imekuja baada ya Tillerson kumaliza ziara yake barani Afrika baada ya kuzuru Ethiopia, Kenya, Chad, Djibouti na Nigeria.

Hata hivyo, Tillerson alisitisha ziara yake barani Afrika baada ya kusema kuwa alikuwa na mambo muhimu ya kwenda kufanya jijini Washington DC.

Rex Tillerson (Kushoto) aliyekuwa Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani katika picha na Mike Pompeo (Kulia) Waziri mpya wa Mamnbo ya nje baada ya kuteuliwa na rais Donald Trump Machi 13 2018 REUTERS/Jonathan Ernst/Aaron P. Bernstein

Yote haya yanakuja wakati huu rais Trump akitarajiwa kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jonn Un mwezi Mei mwaka huu kujadili mradi wake wa nyuklia.

Ripoti zinasema kuwa, Trump alimwarifu Tillerson Ijumaa iliyopita kuwa alikuwa anakwenda kumbadilisha katika nafasi hiyo, lakini hakupewa sababu yoyote.

Wachambuzi wa siasa za Kimataifa wanasema kwa kiasi kikubwa, uamuzi wa Trump umekuja kutokana na mkutano unaopangwa  hivi karibuni kati ya kiongozi wa Marekani na Korea Kaskazini.

Kabla ua uteuzi wake, Tillerson alikuwa mfanyibiashara na Mwenyekiti wa kampuni ya mafuta na gesi ya ExxonMobil, nafasi aliyohudumu kwa muda mrefu.

Mike Pompeo ambaye ni mwananasiasa na afisa wa juu wa Intelejensia nchini Marekani, anatarajiwa kutumia uzoefu wake kumsaidia rais Trump katika utekelezaji wa sera yake ya mambo ya nje.

Kazi ya kuongoza CIA, sasa imemwendea Gina Haspel ambaye alikuwa naibu wa Pompeo.

Haspel anakuwa mwanamke wa kwanza katika historia ya Marekani kuongoza kitengo hicho cha ujasusi nchini Marekani.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana