Pata taarifa kuu
MAREAKNI-URUSI-USHIRIKIANO

Trump: Niko tayari kuhojiwa na kamati ya Mueller

Rais wa Marekani Donald Trump amesema yuko tayari kuhojiwa na Kamati maalum inayochunguza iwapo Urusi iliingia Uchaguzi wa urais nchini humo mwaka 2016.

Rais wa Marekani, DOnald Trump.
Rais wa Marekani, DOnald Trump. REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Trump amesema, anatamani kuhojiwa haraka iwezekanavyo ili kueleza anachokifahamu.

Awali rais Trump alikuwa amenukuliwa akisema kuwa, hakufikiria kuwa angehojiwa na kamati ya Robert Mueller.

Hivi karibuni Rais Donald Trump alisema kuna uwezekano mdogo wa yeye kuhojiwa na Robert Mueller, mkuu wa jopo linalochunguza ikiwa timu ya kampeni ya rais Trump ilishirikiana na Urusi kuingilia uchaguzi wa mwaka 2016.

Kauli ya rais Trump ilikuja baada ya mwanzoni mwa mwezi wa Junuari mwaka huu taarifa kuibuka kuwa mawakili wake wako kwenye mazungumzo na timu ya Mueller kuangalia uwezekano wa yeye kuhojiwa.

Trump ameendelea kusisitiza kuwa yeye hana cha kuficha na kwamba hii ni kampeni mbaya inayofanywa na chama cha Democratic ambacho amesema baada ya kushindwa vibaya kwenye uchaguzi uliopita, wanatafuta mchawi.

Wakati huo huo Urusi imetupilia mbali ripoti ya baraza la Seneti la Marekani ambayo inaishutumu Kremlin kwa kufanya kampeni na kueneza habari zisizo kuwa na msingi wowote ambazo zinalenga kudhoofisha demokrasia, ya nchi hiyo.

Katika Ripoti iliyotolewa hivi karibuni na mwenyekiti wa kamati inayohusika na masuala ya Kidemokrasia na uhusiano wa nje Ben Cardin, ilibainika kuwa Urusi iliingilia Katika uchaguzi wa 2016 Nchini Marekani, kauli ambayo Urusi imekuwa ikikanusha.

Urusi imeendelea kukanusha madai ya kuingilia Uchaguzi huo na kumsaidia Trump kushinda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.