Pata taarifa kuu
MAREKANI-FEDHA

Marekani yakosa fedha za kutoa huduma mbalimbali

Serikali ya Marekani imeanza kufunga baadhi ya taasisi zake baada ya Maseneta kushindwa kukubaliana kuhusu bajeti ya dharura, na hivyo kusababisha baadhi ya shughuli za serikali kukwama.

Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump 路透社
Matangazo ya kibiashara

Mswada uliwasilishwa kwenye Bunge la Senate, lengo likiwa ni kuidhinisha fedha za dharura  ili kuiwezesha serikali kuendelea na shughuli zake na kutoa huduma mbalimbali kufikia mwezi Februari.

Hata hivyo, wabunge wa Democratic walikataa kuunga mkono mswada huo na hivyo kuwafanya wabunge wa Republican kukosa idadi ya Maseneta wanaohitajika kuupitisha.

Badala yake, Maseneta hao waliamua kujadili suala la uhamiaji na kumshtumu rais Trump, kutokana na sera yake kwa madai ya usalama wa Marekani.

Hii ndio mara ya kwanza, tangu mwaka 2013 kwa serikali ya Marekani kujipata katika hali hii kwa siku 16.

Rais Donald Trump amewashtumu Maseneta wa Democratic kwa kuweka mbele suala la uhamiaji badala ya usalama wa nchi hiyo kwa kukataa kuunga mkono mswada huo.

Hali hii itaathiri maelfu ya wafanyikazi wa serikali ambao watachelewa kulipwa mshahara wao na wengine kusalia nyumbani hadi pale shughuli zitakaporejea kama kawaida.

Watu wanaotaka kwenda nje ya nchi, wataathirika kwa sababu kutakuwa na ucheleweshwaji wa kutoa visa.

Mbuga za wanyama na vivutio vingine vya watalii vimefungwa, hatua ambao imeathiri sekta ya utalii nchini humo.

Hata hivyo, huduma katika hospitali na masuala ya usalama zitaendelea kama kawaida.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.