Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Amerika

Watu 12 wafariki katika ajali ya ndege Costa Rica

media Moja ya mitaa ya mji wa San Jose, Costa Rica, ambapo ndege iliyokua ikibeba watalii 10 raia wa Marekaniilio kua ikitokea ikielekea Punta Islita,, ilianguka. REUTERS/Juan Carlos Ulate

Watu 12 ikiwa ni pamoja na 10 raia wa Marekani wamefariki katika ajali ya ndege magharibi mwa Costa Rica, rubani na rubani msaidizi walikua ni raia wa Costa Rica.

Rais wa Costa Rica amethibitisha ajali hiyo katika taarifa iliyochapishwa mitandaoni akisema kuwa serikali yake imesikitishwa sana na vifo hivyo.

Mtangulizi wake rais wa zamani Laura Chinchilla, aliandika katika mtandao wa Twitter kuwa mmoja wa wahudumu wa marubani alikuwa ni binamu wake.

Ripoti zinasema kuwa ndege hiyo ya injini moja ya Cessna 208 Caravan, ilikuwa safarini kutoka mji mkuu San José kwenda Punta Islita ambalo ni eneo la kistarehe.

Mpaka sasa haijabainika chanzo cha ajali hiyo. Watu wote waliokuemo katika ndege hiyo ndogo walifariki.

Vyombo vya habari vimesema kuwa watano kati ya wale waliofariki katika ajali hiyo ni kutoka familia moja.

Hivi karibuni Costa Rica ilikumbwa na kimbunga Nate, kilichosababisha vifo vya watu wengi huku watu 400,000 wakiachwa bila makazi.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana