Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Amerika

Rais wa zamani wa Peru aomba msamaha, Rais Kuczynski ajieeleza

media Waandamanaji wakiandamana katika mji wa Lima dhidi ya kuachiwa huru kwa rais wa zamani wa Peru, Alberto Fujimori. Kwenye bango kumeandikwa "Fujimori muuaji", Peru, Desemba 25, 2017. REUTERS/Mariana Bazo

Kiongozi wa zamani wa Peru, Alberto Fujimori, amewaomba radhi wananchi wa taifa hilo, siku mbili baada ya kupokea msamaha wa rais ambao ulisababisha maandamano mitaani kupinga hatua hiyo.

Akizungumza kupitia video kwenye mtandao wa Facebook iliyorekodiwa akiwa katika kitanda cha hospitali Fujimori amesema anatambua kuwa matokeo ya serikali yake yalipokelewa vizuri kwa upande mmoja, lakini anaikubali kwamba amewaangusha wafuasi wake wengine, na anawaomba kwa dhati, wamsamehe.

Fujimori mwenye umri wa miaka 79 alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 25 kwa makosa ya rushwa na ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanywa wakati akiwa madarakani tangu mwaka 1990 hadi 2000.

Alihamishwa kutoka gerezani hadi hospitali siku ya Jumamosi baada ya kushambuliwa na shinikizo la damu na mabadiliko ya mapigo ya moyo, katika mabadiliko ya hivi karibuni katika mfululizo wa kuugua kwake.

Mapema siku ya Jumapili rais Pedro Pablo Kuczynski aliamuru kuachiwa huru kwa Fujimori na wafungwa wengine saba kwa misingi ya kibinadamu,na kujiweka katikati ya mgogoro wa kisiasa siku chache tu baada ya kunusurika kuondolewa madarakani.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana