Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Amerika

Rais wa zamani wa Peru aachiwa kwa msamaha wa rais

media Rais wa zamani wa Peru Alberto Fujimori alifungwa jela tangu mwaka 2007 na alikuwa amehukumiwa miaka 25 jela kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu, kujipa madaraka na rushwa. REUTERS/Mariana Bazo/Files

Rais wa zamani wa Peru Alberto Fujimori ameachiwa huru kwa msamaha wa rais wa nchi hiyo Pedro Pablo kuczyncski. Taarifa hii ilitolewa saa chache kabla ya ya kuadhimishwa siku ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo (Krismasi).

Rais wa Peru Pedro Pablo Kuczynski amemsamehe rais wa zamani Alberto Fujimori katika misingi ya kiafya katika hatua ambayo imezua maandamano makali.

Kwa mujibu wa afisa wa chama tawala nchini Peru Bw Kuczynski alikubali kumsamehe Alberto Fujimori ili kuzuia kura ya kutokuwa na imani naye, madai ambayo rais Kuczynski amefutilia mbali.

Fujimori ametumikia miaka 10 gerezani wakati ambapo alihukumiwa kifungo cha miaka 25 mwaka 2010 kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu na kuhusika kwa njia moja ama nyingine katika mauaji ya La Cantuta na yale ya Barrios Altos yaliyogharimu maisha ya watu ikiwa ni pamoja na mtoto wa umri wa miaka nane. Wakati huo, vikosi vya serikali viliendesha vita vya kikatili dhidi ya makundi ya waasi ikiwa ni pamoja na kundi la Tupac Amaru. Machafuko yaliyogharimu maisha ya zaidi ya watu 70,000 na wengine kutoweka.

Fujimori pia alihukumiwa miaka sita jela kwa kujiopa madaraka, miaka saba na nusu jela kwa kukubali malipo ya dola Milioni 15 kwa Mkuu wake wa zamani wa Idara ya Ujasusi, Vladimiro Montesinos, na miaka sita jela kwa kupewa hongo kutoka kwa wabunge wa upinzani.

Wakati huo huo polisi katika mji mkuu Lima wamepambana na waandamanaji baada ya kuibuka kwa taarifa iyo ya kuachiwa huru kwa rais wa zamani Alberto Fujimori.

Hata hivyo wafuasi wa Fujimor ambaye aliongoza Peru kuanzia mwaka 1990 hadi mwaka 2000 walisherehekea nje ya hospitali ya serikali ambapo alikuwa akipata matibabu.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana