sikiliza tena
Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Mazungumzo ya amani kuanza Sudan, rais …
Rais wa DRC Felix Tshisekedi akiwa na mwenyeji wake rais wa Tanzania John Magufuli. 13 Juni 2019
 
Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/06 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/06 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/06 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Amerika

UN: Nchi wanachama zakaidi kitisho cha Marekani zapiga kura kuhusu Jerusalem

media Nikki Haley, balozi wa Marekani kwenye umoja wa Mataifa akipiga kura kuzuia azimio lililowasilishwa na Misri REUTERS/Brendan McDermid

Nchi wanachama za umoja wa Mataifa zimekaidi vitisho vya Serikali ya Marekani na kupiga kura ya ndio kuidhinisha azimio linalotupilia mbali tangazo la rais Donald Trump kuutambua mji wa Jerusalem kama makao makuu ya Israel.

Nchi wanachama 128 zilipiga kura ya ndio dhidi ya kura 9 zilizopinga huku nchi 35 zikijiondoa kushiriki kwenye kura hiyo.

Hata hivyo mamlaka ya Palestina imesema licha ya azimio hilo kuungwa mkono, halina nguvu yoyote dhidi ya hatua ya Marekani kuutambua mji wa Jerusalem kama makao makuu ya Israel'.

Tayari nchi kadhaa zimetangaza kupunguza hadhi ya balozi zake nchini Israel kama kuonesha mshikamano na watu wa Palestina.

Azimio hilo limepitishwa licha ya vitisho vya rais Donald Trump ambaye juma hili alitishia kusitisha misaada yake ya kifedha kwa nchi wanachama ambazo zingepiga kura kuunga mkono azimio hilo.

Akizungumza kwenye baraza hilo kabla ya kura yenyewe, balozi wa Marekani kwenye umoja wa Mataifa Nikki Haley aliyaonya mataifa hayo na kusisitiza kuwa Serikali yake haitasahau kitendo cha kidhalimu kilichofanywa na nchi wanachama.

Mpatanishi mkuu wa Serikali ya Palestina Saeb Erakat amelaani uamuzi wa Serikali ya Marekani lakini hata hivyo akapongeza kura hiyo akisema imeonesha umoja wa Mataifa unaheshimu sheria.

Erakat amesema “ni aibu kwa nchi ambazo ziliamua kuunga mkono uamuzi wa Marekani unaifanya Israel kukalia maeneo ya watu kwa nguvu”.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana