Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Amerika

Takwimu: Umri wa kuishi kwa raia wa Marekani wazidi kupungua

media Ofisi ya kitengo cha dawa na chakula nchini Marekani. REUTERS/Jason Reed/File Photo

Umri wa kuishi toka kuzaliwa nchini Marekani umepungua kwa mwaka wa pili mfululizo, ikiwa ni mara ya kwanza kutokea tangu miaka ya 1960, hali iliyochangiwa na matumizi mabya ya dawa.

Kiujumla umri wa kuishi kwa raia wa Marekani katika mwaka 2016 ulikuwa ni miaka 78.6, lakini ulishuka kwa 0.1 kutoka umri wa miaka 78.7 mwaka 2015, imeonesha ripoti ya taasisi ya takwimu za Afya nchini Marekani.

Hii imekuwa ni mara ya kwanza kiujumla kwa umri wa raia wa Marekani kupungua kwa miaka miwili mfululizo tangu mwaka 1962/63 na kabla ya hapo ilitokea tena mwaka 1920.

Mkurugenzi wa kituo hicho Robert Anderson amesema kuwa ‘Kupungua kwa miaka miwili mfululizo ni takwimu za kushtua, na kiashiria kikuu ni kuongezeka kwa matumizi ya kupitiliza ya dawa”.

Mwaka 2016 watu elfu 63 na 600 walikufa kutokana na matumizi mabaya ya dawa, na hii ni kwa mujibu wa kituo cha kupambana na kuzuia magonjwa nchini Marekani.

Vifo vilivyotokana na matumizi mabaya ya dawa mwaka 2016 ilikuwa ni mara tatu zaidi ukilinganisha na mwaka 1999, tatizo ambalo linagusa jinsia zote.

“Tunamatatizo na tunatakiwa tuyashughulikie pamoja kuyaondoa. Matumizi mabaya ya dawa ni suala linalopaswa tuwe na uwezo wa kulizuia na tunapaswa kufanya kitu kuhusu hili’, alisema Anderson.

Umri wa kuishi kwa mwanaume ulikuwa ni miaka 76.1, ikipungua kwa 0.2 kwa mwaka, huku waathirika wakubwa wakiwa sio wale wenye asili ya Hispania, umri wa mwanamke kuishi ulikuwa ni miaka 81.1 mwaka huohuo.

Mwaka 2016 idadi ya vifo nchini Marekani iliongezeka kwa asilimia 9.7 vifo vingi vikitokana na majeraha ya kawaida, asilimia 3.1 kutokana na ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu na asilimia 1.5 watu kujiua.

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana