Pata taarifa kuu
MAREKANI-UCHAGUZI

Mgombea wa chama cha Republican apigwa mweleka katika uchaguzi Alabama

Mgombea wa chama cha Democrats Doug Jones amechaguliwa kuwa Seneta wa jimbo la Alabama katika uchaguzi uliofanyika siku ya Jumanne usiku. Mgombea wa chama cha Democrats alishinda kwa 49.6% ya kura mbele ya mpinzani wake wa chama cha Republican, ambaye alipata 48.9% ya kura.

Mgombea wa chama cha Democrats katika uchaguzi wa Maseneta katika jimbo la Alabama, Doug Jones, wakati wa kampeni ya uchaguzi Birmingham, Alabama, Desemba 10, 2017.
Mgombea wa chama cha Democrats katika uchaguzi wa Maseneta katika jimbo la Alabama, Doug Jones, wakati wa kampeni ya uchaguzi Birmingham, Alabama, Desemba 10, 2017. AFP
Matangazo ya kibiashara

Mgombea wa chama cha Republican Roy Moore ambaye alipewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo majuma kadhaa yaliyopita amekua akikabiliwa na kashfa ya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto. Kushindwa kwa chama cha Republican ni kikwazo kikubwa cha kisiasa kwa Donald Trump, ambaye alikuwa anamuunga mkono Roy Moore, aliyetengwavigogo kadhaa wa chama cha Republican.

Chama cha Democrats kilikua hakijashinda katika jimbo la Alabama tangu mwaka 1992, na tangu wakati huo jimbo hilo lilikua ngome ya chama cha Republican. Doug Jones, mgombea wa chama cha Democrats alimshinda mgombea wa chama cha Republican, Roy Moore, kwa asilimia chache tu ya kura.

Ushindi huu mdogo wa Doug Jones dhidi ya mshindani wake Roy Moore ni sawa na 1% sawa na kura 10,000.

Ushindi huu ni pigo kubwa kwa rais Donald Trump, ambaye alikuwa amewatolea wito wafuasi wake kumuunga mkono na kumpigia kura Roy Moore kwa kuendeleza sera yake ya mageuzi.

Wapiga kura milioni tatu walitakiwa kushiriki uchaguzi kumchagua seneta wao siku ya Jumanne.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.