Pata taarifa kuu
MAREKANI-USALAMA

Wakazi wa New York waingiliwa na wasiwasi kufuatia mlipuko

Hali ya wasiwasi iliripotiwa siku ya Jumatatu Desemba 11 katikati ya mji wa New York baada ya kutokea mlipuko katika handaki inayounganisha eneo la Times Square kwenye na kituo cha magari cha Mamlaka ya Bandari.

Polisi walizuia eneo hilo la tukio karibu na kituo cha magari cha Mamlaka ya Bandari (Authority Port) katikati ya New York kufuatia mlipuko.
Polisi walizuia eneo hilo la tukio karibu na kituo cha magari cha Mamlaka ya Bandari (Authority Port) katikati ya New York kufuatia mlipuko. REUTERS/Edward Tobin
Matangazo ya kibiashara

Mlipuko huo uliwajeruhi watu wanne. Bomu lililotengenezwa kienyeji lililipuliwa na mtu mwenye umri wa miaka 27 aliyejulikana kama Akayed Ullah, mkazi wa Brooklyn. Ni "jaribio la shambulizi la kigaidi," alisema meya wa New York wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Mlipuko ulitokea siku ya Jumatatu asubuhi (saa za Marekani), karibu na kituo cha magari cha Port Authority, kituo cha kinachotembelewa na watu wengi kwa wakati hasa kama huo bomu lilipolipuka.

Kwa mujibu wa mkuu wa polisi James O'Neill, bomu hilo lililipuliwa na mtu mwenye umri wa miaka 27, aliyejulikana kama Akayed Ullah, mkazi wa Brooklyn, ambaye alikua alivalia "kifaa cha kulipuka". Mtu huyo alikamatwa akiwa na "majeraha mwilini" na alipelekwa hospitalini, James O'Neill aliongeza. Watu watatu ambao walikuwa karibu na mtuhumiwa pia walijeruhiwa, ingawa "hakuna aliye katika hali mbaya".

Vyombo vya habari kadhaa vya New York vimeripoti kwamba mtuhumiwa huyo ni kutoka Bangladesh, ambaye aliwasili Marekani. Meya wa New York Bill de Blasio, ametaja kitendo hicho kama "jaribio la shambulizi la kigaidi". Gazeti la kila siku la New York Post likunukuu vyanzo vya polisi, liliarifu kwamba bomu hilo lililipuliwa na dereva wa zamani wa teksi ambaye aliwaambia polisi akiwa hospitali kwamba alifanya hivyo kwa kulipiza kisasi kwa "mashambulizi ya mabomu katika nchi yake", bila kutoa maelezo zaidi.

Mji wa New York umeendelea kusakamwa na mashambulizi ya kigaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.