Pata taarifa kuu
MAREKANI-CALIFORNIA-MAJANGA ASILI

California yaendelea kukumbwa na moto mkubwa wa nyika

Miji mbalimbali ya California nchini Marekani imeendelea kukumbwa na visa vya moto wa nyika. Tayari serikali ya jimbo hilo imeagiza shughuli mpya ya kuhamisha watu baada ya moto mkubwa kushindwa kudhibitiwa siku ya Jumapili kusini mwa jimbo la California.

Moto mkubwa wa nyika waendelea kusababisha uharibifu mkubwa California, Marekani.
Moto mkubwa wa nyika waendelea kusababisha uharibifu mkubwa California, Marekani. REUTERS/Jim Urquhart
Matangazo ya kibiashara

Agizo la kuhama limetolewa usiku wa kuamkia leo Jumatatu sehemu za Carpinteria karibu na msitu wa Los Padres kilomita 160 kutoka Los Angeles.

Vyanzo kadha vya Zima Moto vinasema moto huo wa nyika wa Thomas, unatishia mji wa pwani wa Santa Barbara na mwingine ulio karibu wa Carpinteria.

Awali wazima moto walisema kuwa moto huo ulikuwa unadhibitiwa lakini walishindwa kutokana na ukubwa wa moto huo na kuteketeza eneo lenye ukubwa wa jimbo la Chicago.

Hata hivyo wazima moto hao wanasema moto mwingine katika jimbo hilo umedhibitiwa kwa sehemu kubwa, lakini moto wa Thomas bado unaendelea kuteketez amisitu na umedhibitiwa kwa asilimia 15 tu.

Siku ya Jumamosi Gavana wa California Jerry Brown aliitaja hali hiyo kuwa mpya na kusema kuwa moto huo unaochochewa na mabadiliko ya hali ya hewa utatokea kila mwaka.

Wadadisi wanasema huenda moto huo ukaharibu sekta ya thamani ya mamilioni ya dola ya kilimo katika jimbo la Carlifonia.

Watu 200,000 wamehamishwa kutoka makazi yao katika jimbo hilo na kuharibu nyumba 800, huku mtu mmoja akiripotiwa kufariki na wazima moto kadhaa wamejeruhiwa kufuatia moto huu wa sasa unaoendelea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.