Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 13/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Amerika

Mahakama Kuu Marekani yapitisha marufuku ya Trump kuhusu usafiri

media Un manifestant opposé au décret contre l'immigration de Donald Trump, le 7 février 2017 devant la 9è Cour d'appel de San Francisco. REUTERS/Noah Berger

Mahakama Kuu ya Marekani imeidhinisha agizo la Trump kuhusu marufuku ya usafiri kwa raia kutoka nchi zenye Waislamu wengi. Katika uamuzi wa siku ya Jumatatu, Desemba 4, Mahakama ya Juu nchini Marekani iliruhusu kutekelezwa kwa agizo la rais Trump, ingawa utaratibu wa kisheria bado unaendelea.

Huu ni ushindi wa Donald Trump. Alirekebisha agizo lake mara tatu na kila wakati jaji aliingilia kati kuzuia utekelezaji wake. Lakini siku ya Jumatatu, Mahakama Kuu nchini Marekani ilithibitisha kuwa agizo hilo liko sahihi: Mahakama Kuu iliruhusu utekelezaji kamili wa toleo la hivi karibuni la agizo hilo.

Ni marufuku kwa raia wa nchi nane kusafiri kwenda Marekani. Mwezi Oktoba, majaji wawili wa Marekani waligundua kwamba agizo hilo lina kasoro na ubaguzi wenye misingi ya utaifa. Majaji saba wa Mahakama Kuu kati ya tisa wameamua agizo hilo lianze kutekelezwa , lakini hawakuelezea uamuzi wao.

Hata hivyo, Waislamu, kutoka Libya, Somalia, Chad, Yemen, Syria, na Iran hawataweza kupata visa kwenda Marekani, hata kama wana uhusiano wa familia na watu waishio kisheria nchini Marekani. Korea Kaskazini na Venezuela pia zinahusika, lakini marufuku dhidi ya raia kutoka nchi hizi mbili tayari ilipitishwa na majaji hivi karibuni.

Majadiliano Zaidi yatendelea kusikilizwa wiki hii katika mahakama huko San Francisco, California, na Richmond, Virginia.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana