Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-SIASA

Seneta wa Republican amkosoa Trump kwa kuiangamiza demokrasia Marekani

Rais wa Marekani Donald Trump ameendelea kukukosolewa ndani ya chama chake cha Republican kutokana na msimamo wake tangu tu alipochukua hatamu ya uongozi wa nchi.

Rais Donald Trump akosolewa kudharau maadili ya demokrasia na misingi yake nchini Marekani.
Rais Donald Trump akosolewa kudharau maadili ya demokrasia na misingi yake nchini Marekani. REUTERS/Yuri Gripas
Matangazo ya kibiashara

Seneta wa Chama cha Republican, Jeff Flake, amejiuzulu baada ya kumkosoa Rais Donald Trump.

Jeff Flake ambaye ni Seneta wa jimbo la Arizona amesema hatoacha kumkosoa rais Donald Trump, huku akibaini kwamba siasa za Marekani zimekuwa za kutojali, na tabia ya kujishusha hadhi kutoka ikulu ya Marekani.

Hata hivyo amekosoa desturi ya kudharau maadili ya demokrasia na misingi yake akionya kutokua kama jambo la kawaida kwa baadhi ya viongozi, akimtaja Donlad Trump.

Itafahamika kwamba awali Seneta mwengine wa chama cha Republican, Bob Corker, alimlaumu Rais Donald Trump akisema ni rais ambae sio mwaminifu.

Seneta Jeff Flake amesema hatogombea nafasi yake katika uchaguzi wa mwaka 2018.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.