Pata taarifa kuu
MAREKANI-TABIA NCHI

Moto mkubwa unaoendelea California waua watu 15

Moto mkubwa unaendelea kulikumba jimbo la California, nchini Marekani umeua watu 15, kulingana na ripoti ya awali, na unaendelea kusambaa katika maeneo mbalimbali ya jimbo hili ambapo zoezi la kuhamisha watu linaendelea.

Uharibifu mkubwa uliosababishwa na moto mkubwa unaoendelea California. picha iliyopigwa Oktoba 10, 2017.
Uharibifu mkubwa uliosababishwa na moto mkubwa unaoendelea California. picha iliyopigwa Oktoba 10, 2017. REUTERS/Stephen Lam
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, idadi hii ya atu waliopoteza maisha inaweza kuongezeka katika masaa machache yajayo. Watu 150 bado hawajulikani waliko, kwa mujibu wa gazeti la Washington Post likinuku idara za huduma ya dharura.

Shirika la kuzuia moto la Calfire limetangaza kwamba upepo mkali umekua ukivumaa Jumatano hii, hali ambayo inaweza kuchochea kuongezeka kwa moto huo.

Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza siku ya Jumanne hali ya majanga ya asili na "kuagiza msaada kutoka kwa serikali ya shirikisho kusaidia idara za hudum aya dharura katika jimbo hilo ili kukabiliana na moto huo katika maeneo yaliyoathirika zaidi, kwa mujibu wa taarifa ya ikulu ya White House.

Katika mikoa ya Napa na Sonoma, kaskazini mwa jimbo la San Francisco, nyumba 16,000 zinatishiwa na moto huo.

Jumla ya watu tisa wamepotza maisha katika kata ya Sonoma, wawili katika kata ya Napa na watatu katika kata ya Mendocino. Kwa mujibu wa gazeti la Los Angeles Times, mtu wa kumi na tano aliyepoteza maisha ni kutoka eneo la Yuba, katika kata ya Sutter.

Zaidi ya majengo 2,000 yametetekea kwa moto huo tangu siku ya Jumapili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.