Pata taarifa kuu
MAREKANI-CUBA-USHIRIKIANO

Wanadiplomasia 15 wa Cuba wafukuzwa nchini Marekani

Serikali ya Marekani imechukua uamuzi wa kuwafukuza wanadiplomaisa 15 wa Cuba, ikiishtumu Cuba kwamba haikuwalinda wanadiplomasia wake kutokana na mashambulizi ya kutumia sauti.

Bendera ya Cuba ikinyanyuliwa na umati wa watu mbele ya Ubalozi wa Cuba kabla ya kufunguliwa upya mjini Washington Julai 20, 2015.
Bendera ya Cuba ikinyanyuliwa na umati wa watu mbele ya Ubalozi wa Cuba kabla ya kufunguliwa upya mjini Washington Julai 20, 2015. REUTERS/Gary Cameron
Matangazo ya kibiashara

Cuba imekana kuhusika na swala hilo huku uchunguzi zaidi ukiendelea kujua chanzo cha watu hao kukumbwa na matatizo hayo ya kiafya wanayoyauzungumzia.

Marekani imeiambia Cuba kuwa ina jukumu la kuwalinda wafanyakazi wote wakigeni wakiwemo .

Cuba kupitia Waziri wake wa Mambo ya Kigeni, Bruno Rodriguez, amsema hatua hiyo ya Marekani haikubaliki.

Takriban watu 21 wanaofanya kazi kwenye ubalozi wa Marekani nchini Cuba wamelalamikia matatizo ya kiafya yakiwemo kupoteza uwezo wa kusikia na kizunguzungu.

Ripoti za awali zinasema kuwa mashambulizi ya kutumia sauti ndiyo yalichangia.

Karibu watu 20 raia wa Marekani wamepatwa na matatizo ya kiafya mjini humo.

Mnamo mwezi Septemba Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson alisema Washington inathamini iwapo ifunge ubalozi wake nchini Cuba, baada ya kutokea mlolongo wa mashambulizi ya kelele kwa wafanyakazi wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.