Pata taarifa kuu
MAREKANI-LAS VEGAS-USALAMA

Trump amwita muuaji wa Las Vegas mwendawazimu

Rais Donald Trump wa Marekani amesema mtu aliyehusika na mauaji ya watu 59 na kuwajeruhi wengine 527 katika mji wa Mandalay Bay katika jimbo la Las Vegas ana matatizo ya akili.

Eneo la tukio katika mji wa Las Vegas limefungwa na polisi baada ya mauaji ambayo hayawahi kutokea Marekani, Oktoba 2, 2017.
Eneo la tukio katika mji wa Las Vegas limefungwa na polisi baada ya mauaji ambayo hayawahi kutokea Marekani, Oktoba 2, 2017. REUTERS/Lucy Nicholson
Matangazo ya kibiashara

Polisi inajaribu kubaini dhamira ya Stephen Paddock mwenye umri wa miaka 64 aliwafyatulia risasi watu waliokuwa katika tamasha akiwa katika ghorofa ya 32 karibu na hoteli-casino ya Mandalay Bay.

Polisi iliendesha msako katika chumba cha muuaji huyo na kupata bunduki 23 pamoja na vilipuzi.

Donald trump amesema kuwa ataziangazia upya sheria za umiliki wa bunduki katika siku za usoni lakini hakuelezea zaidi.

Rais Trump ambaye mipango yake kuhusu udhibiti wa bunduki umebadilika katika miaka ya hivi karibuni hakutoa maelezo zaidi.

Saa chahe baada ya shambulio hilo, kundi la Islamic state, kupitia chombo chake cha propaganda cha Amaq, lilitangaza kwamba ndio lilihusika na mauaji hayo.

Hata hivyo maafisa wa usalama nchini Marekani walitupilia mbali madai hayo.

Baadhi ya wachunguzi wamesema kuwa Paddock alikuwa na historia ya matatizo ya kiakili, lakini hilo halijathibitishwa.

Paddock hajakuwa na rekodi yoyote ya uhalifu na hakuwa akijulikana na maafisa wa polisi.

Rais Trump ambaye mipango yake kuhusu udhibiti wa bunduki umebadilika katika miaka ya hivi karibuni hakutoa maelezo zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.