Pata taarifa kuu
MAREKANi-IS-USALAMA

Kundi la IS ladai kutekeleza shambulio la Las Vegas

Kundi la Islamic State(IS) limedai shambulizi lililogharimu maisha ya zaidi ya watu 59 na wengine zaidi ya 200 katika jimbo la Las Vegas, nchini Marekani usiku wa kuamkia siku ya Jumatatu Oktoba 2.

Akitumia kifaa kama nyundo, mshambuliaji aliivunja madirisha ya chumba chake ili aweze kufyatua risasi vizuri, kutoka ghorofa ya 32 ya Hoteli ya Mandalay, Las Vegas.
Akitumia kifaa kama nyundo, mshambuliaji aliivunja madirisha ya chumba chake ili aweze kufyatua risasi vizuri, kutoka ghorofa ya 32 ya Hoteli ya Mandalay, Las Vegas. David Becker/GETTY IMAGES NORTH AMERICA/AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa kundi hili la kijihadi, mshambuliaji "alikua liabadili dini na kuwa Muislam miezi michache iliyopita". Mtu huyo, Stephen Paddock, mwenyeji wa jiji hilo, alijiua kabla ya kuwasili kwa polisi katika eneo alikua amejificha.

Kundi la Islamic State kupitia chombo chake cha propaganda, Amaq, limedai kuhusika na shambulizi hilo liligharimu maisha ya wat wengi katika mji wa Las Vegas, likimtaja mpiganaji wake aliyetekeleza shambulizi hilo kwa jina lake la kivita kama "Abu Abd el-Bir al-Amriki" mwenye umri wa miaka sitini, raia wa Marekani, kuwa ni "mpiganaji wa Islamic State."

Mshambuliaji huyo ambaye alikua alijificha katika moja, alitambulika kwa jina la Stephen Craig Paddock. Alijiua kabla ya polisi kumkaribia. Mshambuliaji huyo alitumia kifaa kama nyundo kwa kuvunja madirisha ya chumba chake ili aweze kutekeleza vizuri kitendo chake hicho kiovu.

Idadi ya vifo ilirekebishwa mara kadhaa na mamlaka husika, na kufikia watu 59 waliouawa na 527 waliojeruhiwa. Ni mauaji makubwa zaidi katika miaka 25 iliyopita nchini Marekani.

Siku ya Alhamisi wiki iliyopita, kiongozi wa IS, Abu Bakr al-Baghdadi, alisikika kwenye mkanda wa video uliorikodiwa akiwataka wapiganaji wake nchini Iraq na Syria kuendelea kupambana na kutoa wito kwa kuendeleza mashambulizi mapya dhidi ya maadui wa kundi la Islamic State. Aliwatolea wito wapiganaji wake na mashujaa wa Uislamu kuendeleza "jihad" na mashambulizi yao. Katika taarifa yake, kundi la Islamic State limeeleza kwamba mashambulizi ya Las Vegas yalifanyika kwa jibu la wito huu.

Kufuatia madai yaliyotolewa na kundi la Islamic State, maafisa wawili waandamizi wa serikali ya Marekani wamesema hakukuwa na kitu chochote kinachoonesha uhusiano kati ya mshambuliaji wa Las Vegas na kundi lolote la kigaidi. FBI imethibitisha kwa upande wake kukosekana "mpaka sasa" uhusiano na kundi la kijihadi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.