Pata taarifa kuu
MAREKANI-MAUAJI

Zaidi ya watu 50 wauawa, 200 wajeruhiwa baada ya kushambuliwa Las Vegas, Marekani

Watu 50 wameuawa na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa baada ya kuvamiwa na kupigwa risasi wakiwa kwenye tamasha la muziki mjini Las Vegas nchini Marekani.

Watu wakijaribu kujikinga na risasi, wakati mshambuliaji alipokua akifyatua risasi hovyo kwenye umati wa watu, Las Vegas, Marekani, Oktoba 2, 2017.
Watu wakijaribu kujikinga na risasi, wakati mshambuliaji alipokua akifyatua risasi hovyo kwenye umati wa watu, Las Vegas, Marekani, Oktoba 2, 2017. David Becker / GETTY IMAGES NORTH AMERICA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Inaripotiwa kuwa mshukiwa aliyetekeleza shambulizi hili baya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini Marekani katika miaka ya hivi karibuni ni Stephen Paddock mwenye umri wa miaka 64.

Aidha, inaelezwa kuwa, mshukiwa huyo alikuwa katika Orofa ya 32 ya hoteli moja na kuwashambulia watu waliokuwa kwenye eneo la wazi wazi karibu na hoteli ya Mandalay Bay wakiburudika.

Mshambuliaji wa Las Vegas alijiua kabla ya polisi kufika katika eneo alipokua kwa mujibu wa Meya wa La Las Vegas.

Mwuaji huyo alikuwa "na silaha nane" katika chumba chake, kwa mujibu wa maafisa wa usalama.

Hofu wakati wa tamasha, lililokumbwa na milio ya risasi Las Vegas.
Hofu wakati wa tamasha, lililokumbwa na milio ya risasi Las Vegas. David Becker / GETTY IMAGES NORTH AMERICA / AFP

Polisi walikuwa wanamshikilia Marilou Danley, mwanamke aliyekuwa anaaminiwa kusafiri na mshukiwa huyo lakini ameachiliwa huru baada ya kubainika kuwa hakuwa na uhusiano wowote.

Mamia ya watu waliokuwa katika tamasha hilo, walianza kutoroka na kukanyagana baada ya kuanza kusikia milio ya risasi huku wakionesha nyuso za wasiwasi na huzuni.

“Tunaweza kusema kuwa zaidi ya watu 50 walipoteza maisha na zaidi ya 200 kujeruhiwa,” amesema Sheriff Joseph Lombardo Mkuu wa jeshi la Polisi mjini Las Vegas.

“Hili ni tukio ambalo hatujawahi kushuhudia,” aliongezea.

Kuamkia Jumatatu asubuhi maduka yamefungwa katika mji huo huku polisi wakiendelea na uchunguzi kubaini iwapo kuwa watu wengine walioshiriki katika tukio hili.

Rais wa Marekani Donald Trump ametuma salamu za rambirambi kwa jamaa, ndugu na marafiki wa watu waliopoteza maisha na kusema shambulizi hilo lilikuwa baya zaid katika historia ya nchi hiyo.

Trump ameongeza kuwa, vyombo vya usalama vinafuatilia karibu tukio hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.