Pata taarifa kuu
MAREKANI-KOREA KASKAZINI-USALAMA

Trump afutilia mbali mazungumzo na Korea Kaskazini

Rais wa Marekani Donald Trump amemuambia waziri wake mambo ya Kigeni Rex Tillerson kuwa anapteza muda wake kwa kufanya mazungumzo na Korea Kaskazini kuhusu mpango wake wa nyuklia.

Rais wa Marekani Donald Trump (kulia) na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un (kushoto).
Rais wa Marekani Donald Trump (kulia) na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un (kushoto). ©SAUL LOEB, Ed JONES / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kauli hii ya Trump inakuja siku mbili tu baada ya Rex kusema kuwa Korea Kaskazini haina nia nzuri ya mazungumzo hayo.

Nchi hizo mbili zimekuwa kwenye majibizano makali miezi ya hivi karibuni.

Rais Trump anatakaKorea Kaskazini kusitisha mara moja mipango yake ya silaha baada ya kufanya majaribio ya makombora zaidi ya sita mwaka huu. Hata hivyo hivi karibuni Korea Kaskazini ilidai kufanya jaribo la bomu la haidrojeni ambalo linaweza kutundikwa kwa kombora la masafa marefu.

Nchi hizi mbili zimeua zikitupia maneno makali, baada ya kila upande kuutumu mwengine kutaka kuhatarisha usalama wa dunia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.