Pata taarifa kuu
MAREKANI-KOREA KASKAZINI-USALAMA

Marekani yaionya Korea Kaskazini

Marekani imeionya Korea Kaskazini, kwa kauli yake “mbovu” kuwa iko tayari kuzidondosha ndege za kivita za Marekani hata kama zipo nje ya anga la taifa hilo.

Rais Trump kupitia ukurasa wake wa twitter, aliandika kuwa utawala wa Korea Kaskazini hauwezi kudumu kwa muda mrefu.
Rais Trump kupitia ukurasa wake wa twitter, aliandika kuwa utawala wa Korea Kaskazini hauwezi kudumu kwa muda mrefu. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini alitoa maneno hayo kufuatia ujumbe wa Rais Trump kupitia ukurasa wake wa twitter, ambapo aliandika utawala wa Korea Kaskazini hauwezi kudumu kwa muda mrefu.

Msemaji wa ikulu ya Marekani ya white House Sarah Huckabee Sanders, amewaambia waandishi wa habari kuwa kauli iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini ni uzushi, wala Marekani haijatangaza vita dhidi ya Korea Kaskazini.

Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Marekani Pentagon Kanal Robert Manning amesema iwapo Korea Kaskazini haitaacha vitendo vyake vya kuudhi,watatoa idhini kwa rais kuchukua hatua dhidi ya Korea Kaskazini.

Naye Waziri wa Mambo ya kigeni wa Korea Kusini Kang Kyung-wha, akizungumza katika kituo cha mafunzo cha kimataifa mjini Washington, amesema dunia inapaswa kutazama njia ya kuepuka maudhi ya Korea Kaskazini.

Bw Kyung-wha amesema Korea Kusini na Umoja wa Mataifa wanapaswa kushughulikia duala la Korea Kaskazini kwa umakini mkubwa, ili kutoendeleza hofu ya madhara ya kijeshi katika ukanda huo.

Wakati huo huo balozi China katika Umoja wa Mataifa Liu Jieyi ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuingilia kati kwani ili kuepuka hali hii ambayo inaingia katika hatua ya hatari.

Korea Kaskazini imesema haitolea mikono iwapo itatishiwa kushambuliwa au kushambuliwa moja kwa moja na nchi yoyote ile, huku ikiapa kuendeleza mpango wake wa nyuklia na majaribio yake ya makombora ya masafa marefu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.