Pata taarifa kuu
FRANCE 24-VYOMBO VYA HABARI

France 24 yapeperusha matangazo yake katika lugha ya Kihispania

Kituo cha kimataifa cha habari cha France 24, kinarusha tangu Jumanne hii Septemba 26 matangazo yake katika lugha ya Kihispania katika eneo nzima la Amerika ya Kusini. Tayari kituo hiki kinarusha matangazo yake katika mabara yote matano katika lunga ya Kifaransa, Kiingereza na Kiarabu.

Kitua cha kimataifa cha habari cha France 24 chazindua lugha ya Kihispania katika matangazo yake.
Kitua cha kimataifa cha habari cha France 24 chazindua lugha ya Kihispania katika matangazo yake. France 24/RFI
Matangazo ya kibiashara

Hatimaye France 24 itasikilizwa na kutazamwa watu wanaozungumza lugha ya Kihispania katika ukanda huo na kwengineko duniani.

Katika hatua ya mwanzo, France 24 inapendekeza kurusha matangazo yake katika lugha ya kwa muda wa saa sita, kila siku kupitia ratiba ya asubuhi na jioni, ratiba ambayo itaendana na programu za lugha ya faransa au Kiingereza. Habari nyingi kwa lugha ya Kihispania zitakua na muoenekano kimataifa na Kifaransakupitia France 24 pamoja na sehemu kubwa itakayozungumzia nchi za Amerika ya Kusini. Makala nyingi za Utamaduni, Uchumi, Historia, Teknolojia mpya, Mazingira na Michezo zitasaidia ratiba ya programu.

Rance 24 katika lugha ya Kihispania ina vifaa na ofisi ya uhariri katika mji wa Bogotá, nchini Colombia, inayoongozwa na mwandishi wa habari Alvaro Sierra na inajumuisha timu ya kimataifa ya waandishi wa habari thelathini ambao wanawakilisha nchi mbalimbali za Amerika ya Kusini.

Chumba cha habari kinapata pia kitasaidiwa na Idha ya Kihispania ya RFI, kituo cha redio cha France Médias Monde, ambacho tayari kinatumika nchini Amerika ya Kusini. Vituo hivi viwili hufanya kazi kwa hasa katika kuandaa pamoja makala mbalimbali, yanayorushwa hewani kwenye televisheni na redio.

France 24 katika lugha ya Kihispania pia utawekwa kwenye ulimwengu wa kidijitali (tovuti, kwenye mpangilio wa simu, mitandao ya kijamii) ili kuwafikishia habari na matukio mbalimbali wasikilizaji na watazamaji wanaozungumza lugha hiyo.

Karibu familia milioni 7 wanaomiliki televisheni katika nchi 12 ameweza kutazama programu za France 24 katika lugha ya Kihispania, bila kusahau familia milioni 12 kutoka Mexico ambao wataweza kutazama kwa muda wa masaa mawili kwa siku kwenye Kituo cha UVTV. Kituo hiki kinapatikana duniani kote kwenye mfiumo wa dijitlil.

Marie-Christine Zaragosse, Mkurugenzi Mkuu wa France Médias Monde, na Marc Saikali, Mkurugenzi wa France 24, walikuwepo katika sherehe ya uzinduzi rasmi wa kituo hiki Jumanne hii Septemba 26 mjini Bogotá na kisha Septemba 28 mjini Buenos Aires. Operesheni hii ya uzinduzi pia itafanyika kabla ya mwisho wa mwaka nchini Mexico na itakuwa fursa ya kuashiria mshikamano wa Framnce Media Monde pamoja na nchi hii iliyokumbwa na tetemeko la ardhi la Septemba 20.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.