Pata taarifa kuu
MEXICO-TABIA CHI

Tetemeko la ardhi Mexico City: Juhudi za uojoaji zaendelea

Watu wasiopungua 225 walipoteza maisha, ikiwa ni pamoja na 86 katika mji mkuu wa Mexico, kulingana na ripoti ya mwisho ya tetemeko la ardhi ambalo lilipiga Mexicona Jimbo la Morelos siku ya Jumanne (Septemba 19).

Waokoaji huingilia kati katika vifusi vya jengo la jengo moja kutafuta waathirika wa tetemeko la ardhi, Mexico City, Septemba 20, 2017.
Waokoaji huingilia kati katika vifusi vya jengo la jengo moja kutafuta waathirika wa tetemeko la ardhi, Mexico City, Septemba 20, 2017. REUTERS/Ginnette Riquelme
Matangazo ya kibiashara

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa 7.1 kwenye kiwango cha Richter, ambapo kina chake kinapatikana kilomita 130 kusini-mashariki mwa mji mkuu, lilisababisha majengo 50 kuporomoka katika nchi hiyo yenye watu milioni 20. Siku moja baada ya tetemeko lenye nguvu, la pili kwa wiki mbili, zoezi la uokoaji likisaidiwa na mamia ya watu wanaojitolea linaendelea ili kupata haraka iwezekanavyo manusura.

Kila dakika inayopita, wasiwasi unaongezeka juu ya hatima ya watoto wa shule ya Enrique Rebsamen ya Mexico City. Watoto ishirini na mmoja walikufa.

Wafanyakazi wa majanga ya dharura na wale wa kujitolewa wamekuwa wakichimbua vifusi kwa kutumia mikono.

Kuna hofu ya watoto zaidi kufariki kutokana na kwamba walikuwa darasani jengo liliporomoka.

Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto amesema kila dakika inahesabika katika kuokoa maisha ya watu.

Watu 52 tayari wameokolewa kutoka katika kufusi katika mji mkuu wa nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.