Pata taarifa kuu
UN-USALAMA

Nchi hamsini zasaini mkataba wa kupiga marufuku silaha za nyuklia

Baadhi ya nchi 50, Brazil ikiongoza, zilitia saini Jumatano hii kwenye mkataba wa kupiga marufuku silaha za atomiki, kitendo cha ishara tu kwa sababu ya kukosekana kwa nakala baada ya kupuuziwa na nchi zenye nguvu ya nyuklia.

Michel Temer , rais wa Brazil, nchi ambayo imeongoza kwa kutia saini kwenye mkataba wa kupiga marufuku silaha za maangamizi.
Michel Temer , rais wa Brazil, nchi ambayo imeongoza kwa kutia saini kwenye mkataba wa kupiga marufuku silaha za maangamizi. Ricardo Botelho/Brazil Photo Press/LatinContent/Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Mkataba huo uliandikwa mwezi Julai na nchi 122. Utaanza kutekelezwa mara tu utadhinishwa na nchi 50.

Mataifa tisa yenye nguvu ya nyuklia hazitaki kujiunga na mkataba huo. Rais wa Brazil Michel Temer alikua wa kwanza kusaini mkataba huo, na alifuatiwa na nchi nyingine 50. Hakuna kat ya nchi yisa zenye nguvu yanyuklia, Marekani, Urusi, China, India, Pakistan, Israel, Ufaransa, Uingereza, na Korea Kaskazini, ambazo zilipanga kujiunga na mkataba huo. Nchi wanachama wa Jumuiya ya kujihami ya nchi za magharibi (NATO) pia zilijiweka kando, pamoja na Japan, nchi pekee ambayo ilikumbwa na mashambulizi ya silaha ya atomiki mwaka 1945.

"Tunapaswa kuwa wa kweli". Marekani, Ufaransa na Uingereza, wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, mara kadhaa walikosoa jitihada hizo katika miezi michache iliyopita, wakitoa mfano wa mgogoro wa Korea Kaskazini kama mfano wa wa kujitenga mbali na zilaha za maangamizi. "Hakuna kitu ninachotaka kwa familia yangu na ulimwengu kama kutokua silaha za nyuklia, lakini tunapaswa kuwa wa kweli. Ni nani anayeweza kuamini kwamba Korea Kaskazini ingekubali kupiga marufuku silaha za nyuklia?" amesema mnamo mwezi Machi balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, Nikki Haley.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.