Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/07 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/07 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/07 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Amerika

Mazungumzo kati ya serikali ya Venezuela na upinzani yaendelea Santo Domingo

media Spika wa Bunge jipya la Katiba la Venezuela, Delcy Rodriguez (wa pili kutoka kushoto) na Jorge Rodriguez (kulia), kiongozi wa Chama cha Kisoshalisti cha kinachounga mkono serikali ya Venezuela, katika mkutano wa waandishi wa habari Santo Domingo, Dominika. AFP

Wajumbe wa serikali ya Venezuela na upinzani wanaendelea Alhamisi hii nchini Jamhuri ya Dominika kuweka sawa ajenda ya mazungumzo ya kutatua mgogoro wa kisiasa unaoendelea kuikabili nchi yao, amesema Rais wa Jamhuri ya Dominika Danilo Medina.

"Tuko katika mchakato wa maendeleo, na kutengeneza ajenda inayoelekea kwa majadiliano ya mwisho ya mgogoro," amesema rais Madina, katika hutuba fupi kwa vyombo vya habari mwishoni mwa mkutano na wajumbe wote kutoka pande mbili husika katika mgogoo huo katika moja ya majengo ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Dominika.

Mazungumzo yamepangwa kuanza tena Alhamisi hii saa 9:00 asubuhi saa za Jamhuri ya Dominika (sawa na saa saba kamili saa za kimataifa), rais Madina ameongeza.

"Kitu pekee ninachoweza kusema usiku wa leo ni kwamba tumesikiliza pande zote na wamejieleza na kutoa maoni yao juu ya hali inayoendelea nchini Venezuela," amesema rais wa Jamhuri ya Dominika, ambaye pia alikutana na waziri mkuu wa zamani wa Uhispania, José Luis Rodriguez Zapatero, mmoja wa waanzilishi wa majadiliano kati ya Wavenezuela.

Wawakilishi wa serikali ya Kisoshalisti ya Caracas na upinzani walikutana siku ya Jumatano katika Jamhuri ya Dominikai katika jaribio jipya la kutatua mgogoro mkubwa wa kisiasa.

Ujumbe wa rais Nicolas Maduo umesemakuwa una na matumaini makubwa kwa mazungumzo hayo.

"Naweza kusema kwamba tuko karibu sana na kutatua pointi nyingi ambazo ziko kwenye ajenda, na ambazo zitakua katika ajenda ya mazungumzo siku ya leo," Jorge Rodriguez, aliyetumwa na serikalikushiriki mazungumzo haya aliwahakikishi waandishi wa habari.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana