Pata taarifa kuu
MAREKANI-TABIA NCHI

Donald Trump kuzuru maeneo yalioathirika na kimbunga Irma Florida

Donald Trump anatarajia kutembelea Alhamisi hii katika maeneo yaliyoathirika na kimbunga Irma katika jimbo la Florida, hasa katika eneo la "Sunshine State" ambapo watu wanane walipoteza maisha, labda kwa sababu ya ukosefu wa umeme.

Kimbunga Irma kilibadilika kuwa dhoruba ya kitropiki kilichosababisha mafuriko katika miji kadhaa. Hapa ni katika mji wa Naples, Septemba 11, 2017.
Kimbunga Irma kilibadilika kuwa dhoruba ya kitropiki kilichosababisha mafuriko katika miji kadhaa. Hapa ni katika mji wa Naples, Septemba 11, 2017. REUTERS/Stephen Yang
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani aanatarajiwa katika maeneo ya fukwe ya Naples na Fort Myers, katika pwani ya magharibi ya rasi, eneo lililoathirika zaidi na kimbunga cha kutisha ambacho kimesabababisha vifo vya watu ishirini katika jimbo la Florida.

Donald Trump alitangaza siku ya Jumapili kwamba atazuru jimbo lililoathirika zaidi kama alivyofanya katika jimbo la Texas lililokumbwa mwishoni mwa mwezi Agosti na mafuriko ya kihistoria kutokana na kimbunga Harvey, katika hali ya kuonyesha kuwa yuko karibu na waathirika, moja ya kazi yake kama rais ambayo inameahidi kutekeleza.

Wazee wanane waliokua wakiishi katika nyumba ya serikali walipoteza maisha katika jimbo la Florida, labda kutokana na ukosefu wa hali ya hewa katika makazi yao siku tatu baada ya kimbunga Irma kupiga jimbo hilo. Kimbunga Irma kimesababisha uharibifu mkubwa na kuacha mamilioni ya watu bila umeme.

Wazee hao waliokua wakiishi katika nyumba hiyo kaskazini mwa Miami, katika mji wa Hollywood, wenye umri wa miaka 70 hadi 99, wanaweza kuwa waathirika wa mwisho wa kimbunga Irma na kufikisha idadi ya watu 20 waliopoteza maisha. Kimbunga hiko kilua watu wengine 40 katika visiwa vya Caribbean.

Ukosefu wa umeme na hali ya hewa, vinaweza kuwa sababu ya vifo vya wazee hao, alisema mkuu wa polisi wa eneo hilo aliyenukuliwa na kituo cha CNN kuhusu waathirika sita wa kwanza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.