Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 13/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Amerika

Mahakama ya Juu Marekani yataka zuio la wakimbizi kutekelezwa

media Rais wa Marekani, Donald alitoa agizo la kupiga marufu raia kutoka nchi sita za Kiislam kuingia nchini Marekani. REUTERS/Jonathan Ernst

Mahakama ya juu nchini Marekani imesisitiza kutekelezwa kwa amri ya utawala wa rais Donald Trump kuhusu zuio la wakimbizi kuingia nchini humo, hatua ambayo kwa muda imezima matumaini ya wakimbizi elfu 24 ambao wameidhinishwa kama wahamiaji.

Majaji wa mahakama ya juu nchini humo walikubali rufaa ya dharula iliyowasilishwa na serikali kupingwa kutekelezwa kwa amri ya mahakama ya San Francisco ambayo licha ya kuidhinisha amri ya rais Trump ilikuwa imeruhusu maelfu ya wahamiaji kuingia nchini humo licha ya zuio.

Uamuzi huu wa mahakama ya juu kukubali rufaa ya serikali unamaanisha kuwa sasa wahamiaji wote waliokuwa wameomba kibali cha kuingia nchini humo itawabidi wasubiri hadi pale rufaa ya serikali itakapopitiwa upya Oktoba 10.

Septemba 8 mwaka huu mahakama mjini Francisco ilitoa uamuzi ambao ulisema zuio la serikali halikuwahusu wahamiaji ambao tayari walikuwa wamepewa hakikisho la kuingia nchini humo.

Zuio hili la rais Trump lilihusu raia wanaotoka kwenye mataifa 6 ya kiislamu

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana