Pata taarifa kuu
CARABBEAN-IRMA-TABIA NCHI

Idadi ya vifo yaongezeka kufuatia kimbunga Irma katika visiwa vya Caribbean

Irma, kimbunga kikali zaidi kilichoorodheshwa katika Atlantiki, kinaendelea kusababisha uharibifu mkubwa katika visiwa vya Caribbean. Idadi ya vifo vilivyotokea usiku wa Ijumaa Septemba 8, pamoja na vifo vya watu wasiopungua 14 katika mji wa St Martin, katika visiwa vya Virgin, katika mji wa Puerto Rico na Barbuda.

Polisi wakikagua hasara iliyosababishwa n akimbunga Irma Septemba 7, 2017 Nagua, Jamhuri ya Dominika.
Polisi wakikagua hasara iliyosababishwa n akimbunga Irma Septemba 7, 2017 Nagua, Jamhuri ya Dominika. REUTERS/Ricardo Rojas
Matangazo ya kibiashara

Upepo pengine uyolizidi kilomita 300 / h umesababisha uharibifu mkubwa katika miji ya Saint-Martin na Saint-BarthΓ©lemy, ambako wakazi bado wamekosa umeme. Hakuna taarifa yoyote kutoka visiwa vya Turks na Caicos, visiwa vidogo vya Caribbean ambavyo vilikumbwa na kimbunga Irma.

Ni vigumu kuelezea hali hali kuhusu kimbunga Iram akatika baadhi ya visiwa vya Carabbean. Kisiwa cha Barbuda kiliharibiwa kabisa kwa mujibu wa Waziri Mkuu Gaston Browne.

Upepo wenye kasi kufikia kilomita 360 kwa saa ulivuma katika visiwa vya Saint-BarthΓ©lemy na Saint-Martin. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ufaransa imetangaza idadi ya watu wasiopungua 9 walipoteza maisha, 7 walipotea, na 112 walijeruhiwa ambapo wawili wako katika hali mbaya katika visiwa hivi viwili vinavyomilikiwa na Ufaransa.

Kati ya watu 50 waliojeruhiwa ambao waliorodheshwa, wawili wako katika hali mbaya. Uharibifu ni mkubwa sana. Katika kisiwa cha Saint-Martin, kwa upande wa Ufaransa, mamlaka imeelezea kuguswa na hali hiyo na kubaini kwamba kimbunga Irma kimesababisha uharibifu unaokadiriwa kufikia 95 % katika kisiwa hiki, ambacho kimekosa umeme, maji safi na petroli. Barabara karibu zote zimeharibika.

Visa vya uporaji vyashuhudiwa

Jumla ya wajeshi 455 wamewasili eneo hilo kusaidia maelfu ya waathirika, lakini pia ili kuzuia uporaji wa chakula kwa watu binafsi na katika maduka makubwa. Kikosi kipya cha askari 187 kimetumwa katika kisiwa hiki wakati wa mchana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.