Pata taarifa kuu
HAITI-MAREKANI-TABIA NCHI

Kimbunga Irma chaelekea Puerto Rico

Baada ya kuharibu sehemu ya West Indies, kimbunga Irma kinatishia Puerto Rico. Nchini Haiti, athari za kwanza za kimbunga hiki zinatarajiwa kwa saa za mwanzo za Alhamisi hii.

Kimbunga Irma chasababisha uharibifu mkubwa katika visiwa vya Caribbean.
Kimbunga Irma chasababisha uharibifu mkubwa katika visiwa vya Caribbean. HECTOR RETAMAL / AFP
Matangazo ya kibiashara

Nchi nzima iko katika tahadhari nyekundu lakini pwani ya kaskazini inakabiliwa na hatari zaidi na inaweza kukabiliana na upepo wa kilomita zaidi ya 200.

Kimbunga hiki kimeharibu majumba na kusababisha vifo na mafuriko makubwa katika visiwa vya Caribbean.

Kisiwa kidogo cha Barbuda kilisemekana kukumbwa na uharibifu mkubwa hadi kutajwa kuwa kisichoweza kukalika huku maafisa wakionya kuwa himaya ya Uingereza ya St Martin imeharibiwa kabisa.

Majumba manne "imara zaidi" katika visiwa vya Saint Martin, ambavyo humilikiwa na Ufaransa na Uholanzi, yameharibiwa, waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Gérard Collomb amesema.

Kimbunga hicho kina upepo unaovuma kwa kasi inayofikia 295km/h.

Kimbunga Irma cha kiwango cha tano, ambacho ni kiwango cha juu zaidi kwa sasa kinapita kaskazini mwa Puerto Rico.

Zaidi ya nusu ya wakaazi wote milioni tatu wa Puerto Rico hawana umeme baaada ya kimbunga Irma kusababisha mvua kubwa na upepo mkali. Maafiasa wanasema huenda umeme ukakosa kwa siku kadhaa.

Jitihada za uokoaji zinatatizwa kutokana na kuwepo ugumu wa kuyafikia maene mengine.

Itafahamika kwamba baadhi ya maeneo ya Texas na Louisiana yanakabiliana na uharibifu uliotokana na Kimbunga Harvey mwishoni mwa Agosti.

Kufikia sasa haijabainika Kimbunga Irma kitakuwa na uharibifu kiasi gani Marekani bara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.