Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Amerika

Obama akosoa hatua ya rais Trump kufuta kinga ya wahamiaji

media Aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama akizungumzia kuhusu wahamiaji wakati alipotembelea eneo la Casa Azafran mjini Nashville. Picha ya maktaba. December 9, 2014. REUTERS/Kevin Lamarque/File Photo

Wanasiasa nchini Marekani wamemjia juu rais Donald Trump baada ya kutangaza kufuta msamaha wa kinga iliyokuwa imetolewa na mtangulizi wake Barack Obama kwa raia zaidi ya laki 8 walioingia nchini humo wakiwa na umri wa chini ya miaka 16.

Wafanyabiashara, mashirikisho ya wafanyakazi, viongozi wa dini, wanasiasa wa upinzani kutoka chama cha Democrats na wengi kutoka chama cha rais Trump cha Republican wameungana kukosoa uamuzi wake.

Raia hao ambao wengi ni wa latino wana umri wa miaka 20 hivi sasa watakuwa na muda wa miezi sita hadi 24 kabla ya kutambuliwa kama raia wanaoishi nchini humo kinyume cha sheria na huenda wakarudishwa kwa nguvu nchini mwao.

Vijana wengi ambao waliingia Marekani wakiwa watoto wanasema wanashangazwa na uamuzi huu wa rais Trump waliosema ni kinyume na utu na kuapa kutoondoka nchini humo bila kupigania haki.

Baadae rais Trump alijitokeza na kudai kuwa ana upendo kwa raia hao na kulitaka bunge la Congress kupitisha sheria kadhaa za mabadiliko kuhusu wahamiaji jambo ambalo watunga sheria hao wameshindwa kufanyia marekebisho sheria hiyo kwa miongo kadhaa.

Rais Trump ameandika kwenye mtandao wao wa Twitter kuwa analenga kufanya kazi kwa pamoja na wanasiasa wa pande zote mbili ili kuleta sheria ambazo zitawalinda kwanza raia wa Marekani kabla ya wageni.

Trump kwenye amri yake amesema kuwa msamaha huo uliotolewa na rais Barack Obama mwaka 2012 ulikuwa kinyume cha katiba na ulivuka mipaka ya madaraka ya rais.

Kwa upande wake rais Barack Obama amemshambulia rais Trump na utawala wake kwa kutengua amri aliyokuwa ametangaza ya kuwalinda vijana walioingia nchini humo wakiwa watoto bila kuwa na nyaraka.

Msamaha huu uliokuwa unafahamika kama Daca umetenguliwa hapo jana na rais Trump katika uamuzi ambao huenda ukaathiri zaidi ya wanufaika wa msamaha huo laki 8.

Akitoa wito kwa wabunge wa Congress rais Obama amesema uamuzi wa rais Trump “hauna utu na “hauko sahihi”, huku akiwataka wabunge hao kutupilia mbali muswada huo pindi utakapowasilishwa bungeni.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana