Pata taarifa kuu
MAREKANI-HALI YA HEWA

Donald Trump azuru Texas baada ya kimbunga Harvey

Siku ya Jumanne Rais Donald Trump alizuru Texas, moja ya majimbo ya Marekani ambayo yanaendelea kukumbwa na kimbunga Harvey. Katika ziara hiyo Bw Trump aliambatana na mkewe Melania Trump pamoja na viongozi wengine serikalini ili kutathmini uharibifu uliofanywa na kumbunga hicho.

Rais wa Marekani na mkewe Melania, baada ya kuwasili Austin, mji mkuu wa Texas, kusaidia watu walioharibiwa na kimbunga Harvey Jumanne, Agosti 29.
Rais wa Marekani na mkewe Melania, baada ya kuwasili Austin, mji mkuu wa Texas, kusaidia watu walioharibiwa na kimbunga Harvey Jumanne, Agosti 29. REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Kwa sasa baadhi ya maeneo ya Texas yamekumbwa na mafuriko kutokana na mvua zilizonysha kwa wingi siku chache zilizopita. Kimbunga Harvey kimevunja rekodi kwa kiwango kikubwa cha mvua katika siku chache zilizopita.

Donalt Trump amewahakikishia watu walioathiriwa na mvua hizo kuwa serikali itawasaidia.

Katika eneo la Corpus Christi mahali ambako awali kulishuhudiwa hali ya hatari kufuatia kimbunga Harvey, Bw Trump aliwashukuru wafanyakazi wa vitengo vya dharura ambao walikuwa wakikabiliana na mafuriko. Donald Trump amewapongeza akisema walifanya kazi kubwa ambayo kila mtu ameisifu.

Wakati huo huo katikamji wa Houston, mabwawa mawili yameanza kufurika , na kumeshuhudiwa kuongezeka kwa mafuriko makubwa.

Gavana wa jimbo la Texas , Greg Abbott, amemtaka rais Trump kutambua changamoto kubwa zinazoukabili mji wa Texas, huku akisema kwamba mji wake umeomba msaada wa dharura kutoka serikali kwa watu wengine elfu kumi kupatiwa makazi ya dharura.

Donald Trump alirudi Washington jioni. Sasa anapaswakutekeleza ahadi zake na kupata fedha muhimu kutoka kwa idhini ya Bunge la Congress.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.