Pata taarifa kuu
MAREKANI-MEXICO

Trump asema anaweza kusitisha shughuli za serikali kujenga ukuta mpakani na Mexico

Rais wa Marekani Donald Trump amesema atasitisha shughuli za serikali, kama itamlazimu ili kujenga ukuta katika mpaka wa nchi jirani Mexico.

Rais Donald Trump, akiwahotubia wananchi  mjini  Phoenix, jimboni  Arizona.
Rais Donald Trump, akiwahotubia wananchi mjini Phoenix, jimboni Arizona. REUTERS/Joshua Roberts
Matangazo ya kibiashara

Trump ametoa kauli hii wakati akiwahotubia mkutano wa hadhara jimboni Arizona.

Aidha, amesema ataliomba bunge la Congress kupitisha mswada wa kumpa fedha za kujenga ukuta huo ambao amesema utakuwa mkubwa na wa kupendekeza.

Trump amekuwa akisema hata kabla ya kuchaguliwa kuwa, atajenga ukuta huo kwa lengo la kuwazuia wahamiaji haramu wanaoingia Marekani.

Wakati uo huo, Trump amevilaumu vyombo vya Habari nchini humo kwa kuyapa nafasi makundi yenye mrengo wa kulia, kuzua wasiwasi nchini humo.

Hivi karibuni, kumekuwa na mapigano kati ya watu wenye mirengo tofauti na ya kibaguzi.

Kamati ya Umoja wa Mataifa imesema suala hili linastahili kutafutiwa ufumbuzi wa haraka ili kuepuka mapigano na mauaji zaidi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.