Pata taarifa kuu
MAREKANI-KOREA KASKAZINI-USALAMA

Trump aisifu Korea Kaskazini kwa kuheshimu onyo lake

Rais Donald Trump amesema kuwa Korea Kaskazini imeanza kuwaheshimu, huku akisema kuwa kuna matumaini kuhusu kupungua kwa wasiwasi uliokuwepo kati ya Marekani na Korea kaskazini.

Donald Trump aionya Korea Kaskazini kwamba "itakiona cha mtima kuni" iwapo itatenda lolote kwa Marekani.
Donald Trump aionya Korea Kaskazini kwamba "itakiona cha mtima kuni" iwapo itatenda lolote kwa Marekani. REUTERS/Joshua Roberts
Matangazo ya kibiashara

Bw Trump azungumza hayo saa chache baada ya Korea Kaskazini kutangaza kwamba ina mpango wa kurusha makombora manne karibu na kisiwa cha Marekani cha Guam.

“Kim Jong un Ninaheshimu ukweli kwamba ameanza kutuheshimu, “ Rais Donald Trump amesema.

Awali Donald Trump aliionya Korea Kaskazini kwamba "itakiona cha mtima kuni" iwapo itatenda lolote kwa Marekani.

Hivi karibuni Trump alisema utawala wa Korea Kaskazini utapatwa na shida kubwa ambayo ni mataifa machache yaliyowahi kukumbana nayo iwapo wataendelea na mpango wao.

Korea Kaskazini imesema mpango wake wa kufyatua makombora kwenda kisiwa cha Marekani cha Guam, utakuwa tayari hivi karibuni. Hata hivyo viongozi wa nchini hizi mbili wameendelea kutoleana maneno ya kivita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.