Pata taarifa kuu
MAREKANI-CHINA-URUSI-UCHUMI

Marekani yatangaza vikwazo dhidi ya makampuni ya China na Urusi

Marekani imeweka vikwazo dhidi ya makampuni kadhaa ya Urusi na China na watu ambao inawashtumu kusaidia mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.

Kiongozi wa Korea Kim Jong-un,katika picha iliyotolewa Mei 28, 2017.
Kiongozi wa Korea Kim Jong-un,katika picha iliyotolewa Mei 28, 2017. KCNA/via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

China iimejibu kwa kutoa wito kwa Marekani ikitaka irekebishe makosa yake ya kuadhibu makampuni ya China.

Wizara ya fedha nchini Marekani ilisema kuwa vikwazo hivyo vitaongeza shinikizo kwa Korea Kaskazini lakini hatua hiyo imeighadhabisha China.

Wizara ya fedha itaendelea kuongeza shinikizo kwa Korea Kaskazini kwa kulenga wale wanaosaidia kuendelea kwa mipango ya nyuklia na ya makombora ya masafa marefu.

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Rex Tilleron, wakati huo huo ameipongeza Korea Kaskazini kwa kujizuia siku za hivi karibuni.

Hivi karibuni baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa, zikiwemo Urusi na China walipiga kura ya kuiwekea viwazo zaidi Korea Kaskazini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.