Pata taarifa kuu
MAREKANI-AJALI-USALAMA

Manowari ya Marekani yagongana na meli ya mafuta

Manowari ya Marekani imegongana na meli ya mafuta katika pwani ya Singapore. Wanajeshi 10 hawajulikani waliko na wengine watano wamejeruhiwa baada ya ajali hiyo.

Manowari ya Marekani USS Curtis Wilbur, amnbayo ni ndogo kwa ile ya USS John S. Cain.
Manowari ya Marekani USS Curtis Wilbur, amnbayo ni ndogo kwa ile ya USS John S. Cain. REUTERS/U.S. Navy/Mass Communication Specialist 3rd Class Declan
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa jeshi la wanamaji la Marekani wanajaeshi kumi hawajulikani waliko na watano wamejeruhiwa baada ya Manowari ya Marekani USS John S. McCain kugongana na meli ya mafuta. Ajali hiyo ilitokea siku ya Jumatatu mashariki mwa Singapore.

Shughuli kubwa ya kuwatafuta na kuwaokoa wanajeshi inaendelea.

Manowari ya USS John S. McCain ilikuwa mashariki mwa Singapore ikijiandaa kutia nanga bandarini wakati iligongana na meli iliyokuwa ikipeperusha bendera ya Liberia.

Helikopta za jeshi la Marekani na jeshi la Singapore pamoja na walinzi wa pwani, wanafanya shughuli za uokoaji. Malaysia nayo imejiunga katika shughuli hiyo.

Meli hiyo ya mafuta inaripotiwa kuwa na uzito mara tatu wa manowari ya jeshi ya USS John S. McCain, na taarifa zinasema kuwa haikuwa imebeba mafuta wakati ya ajali hiyo.

Itakumbukwa kwamba mwezi Juni mabaharia saba wa Marekani waliuawa wakati manowari ya USS Fitzgerald iligongana na meli ya mizigo kwenye bahari ya Japan karibu na bandari ya Yokosuka.

Hili ni tukio la pili kubwa linaloikumba meli ya jeshi la wanamaji wa Marekani miezi ya hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.