Pata taarifa kuu
VENEZUELA-KATIBA-HAKI

Venezuela yashtumiwa na nchi 12 za Amerika

Nchi 12 za Amerika zimeishtumu serikali ya Venezuela kuvunja demokrasia, huku Umoja wa Mataifa ukilaani "matumizi ya nguvu" wakati wa maandamano dhidi ya Rais Nicolas Maduro.

Umoja wa Mataifa ukilaani "matumizi ya nguvu" wakati wa maandamano dhidi ya Rais Nicolas Maduro
Umoja wa Mataifa ukilaani "matumizi ya nguvu" wakati wa maandamano dhidi ya Rais Nicolas Maduro REUTERS/Ueslei Marcelino
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa nchi hizi 12 za Amerika, hususan Argentina, Brazil, Canada, Chile, Colombia, Costa Rica, Guatemala, Honduras, Mexico, Panama, Paraguay na Peru, walikutana katika mji wa Lima, na kutangaza uamuzi wao wa kutolitambua Bunge la Katiba, lililochaguliwa hivi karibuni au maamuzi litakalochukua.

Katika waraka uliyotolewa mwishoni mwa mkutano uliodumu saa sabakatika mji mkuu wa Peru, viongozi hao walisem awataendelea kuunga mkono na kuonyesha mshikamano wao kwa Bunge, linalodhibitiwa na upinzani.

Pia wameshtumu "ukosefu wa uchaguzi huru, vurugu, ukandamizaji, na kuwepo kwa wafungwa wa kisiasa."

Wakjati huo huo rais wa Venezuela amependekeza "mazungumzo ya kikanda" na nchi hizi ili "kurejesha viwango vya heshima kwa sheria za kimataifa."

Bw Maduro alitoa tangazo hili katika mji wa Caracas siku ya Jumanne wakati wa mkutano na washirika wake wachache, ikiwa ni pamoja na Cuba, Bolivia, Nicaragua na Ecuador.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.