Pata taarifa kuu
MAREKANI-URUSI-USHIRIKIANO-VIKWAZO

Donald Trump apitisha vikwazo dhidi ya Urusi

Rais wa Marekani Donald Trump ameusaini kuwa sheria mswada ambao utaiwekea vikwazo vipya Urusi, kwa kuingilia katika uchaguzi wa Marekani mwaka 2016. Uamuzi huo umechukuliwa baada ya Baraza la Seneti la Marekani kuidhinisha vikwazo hivyo licha ya pingamizi la awali la White House.

Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, mjini Hamburg, Julai 7, 2017.
Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, mjini Hamburg, Julai 7, 2017. REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Mswada huo pia unaziwekewa viwazo Iran na Korea Kaskazini.

Vikwazo hivyo ni vya kuiadhibu Urusi zaidi kufuatia hatua za kulimega eneo la Crimea kutoka Ukrain mwaka 2014.

Bunge la Congress liliidhinisha mswaada huo mapema wiki jana kwa kura nyingi.

Sheria hiyo inamzuia Trump kutokana na kuipunguzia vikwazo Urusi bila ya idhini ya bunge la Congress.

Uchunguzi kuhusu hatua za Urusi kuingilia kati uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2016 ukiendelea.

Rais Donald Trump mara nyingi amekana kuwa Urusi iliingilia uchaguzi huo kusaidia kampeni yake na kumuangusha mshindani wake Hillary Clinton, aliyekua mgombea wa chama cha Democratic katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2016.

Kwa kujibu vikwazo hivyo mapem awiki iliyopita rais wa Urusi Vladimir Putin alitoa agizo kwa wanadiplomasia 755 wanaohudumu kwenye ubalozi wa Marekani nchini Urusi kuondoka katika ardhi ya Urusi kufikia Septemba mosi.

Urusi iliidhinisha hatua hiyo kwa ghadhabu kufuatia vikwazo vipya vilivyopitishwa na bunge la Marekani dhidi yake, kwa tuhuma za kuingilia uchaguzi wa taifa hilo mwaka jana.

Rais Vladimir ameapa kuwa upo uwezekano wa kuongeza vikwazo zaidi dhidi ya serikali ya Marekani.

Rais Putin alisema kuwa alitarajia uhusiano baina ya Moscow na Washington ungebadilika na kuwa mzuri, lakini hilo haliwezekani kwa sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.