Pata taarifa kuu
MAREKANI-URUSI-USHIRIKIANO-VIKWAZO

Bunge la Senate lapiga kura ya vikwazo dhidi ya Urusi, Iran na Korea Kaskazini

Bunge la Senate nchini Marekani limepitisha vikwazo vipya dhidi ya Urusi, Iran na Korea Kaskazini licha ya rais Donald Trump kupinga.

Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, mjini Hamburg, Julai 7, 2017.
Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, mjini Hamburg, Julai 7, 2017. REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Vikwazo hivyo ni vya kuiadhibu Urusi zaidi kufuatia hatua za kulimega eneo la Crimea kutoka Ukrain mwaka 2014.

Baada ya mswaada huo kupita katika mabunge yote sasa utapelekwa kwa Rais Donald Trump kuwekwa sahihi.

Hata hivyo Trump anataka kuboresha uhusiano na Urusi na anaweza kuukataa licha na uungwaji mkono uliopata.

Wachanganuzi wa masuala ya siasa wanasema kuwa ikiwa Trump atajaribu kuukataa mswaada huo basi itakuwa ishara tosha kuwa anaiunga mkono Urusi.

Bunge la Congress liliidhinisha mswaada huo mapema wiki hii kwa kura nyingi.

Mjadala kuhusu vikwazo hivyo vipya unafanyikawakati ambapo uchunguzi kuhusu hatua za Urusi kuingilia kati uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2016 ukiendelea.

Rais Donald Trump mara nyingi amekana kuwa Urusi iliingilia uchaguzi huo kusaidia kampeni yake na kumuangusha mshindani wake Hillary Clinton, aliyekua mgombea wa chama cha Democratic katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2016.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.