Pata taarifa kuu
MAREKANI

Msemaji wa rais Trump ajiuzulu

Sean Spicer msemaji wa rais wa Marekani Donald Trump amejiuzulu.

Aliyekuwa msemaji wa Ikulu ya Marekani  Sean Spicer akiwa katika mkutano wake wa mwisho Julai 17 2017
Aliyekuwa msemaji wa Ikulu ya Marekani Sean Spicer akiwa katika mkutano wake wa mwisho Julai 17 2017 REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa Spicer aliamua kujiuzulu kwa sababu hakufurahishwa na uamuzi wa rais Trump kumteua Mkurugenzi mpya wa mawasiliano katika mpangilio mpya katika idara ya Mawasiliano.

Inaelezwa kuwa Anthony Scaramucci mfadhili wa kampuni ya Wall Street ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa mawasiliano katika Ikulu hiyo.

Spicer mwenye umri wa miaka 45, amesema amemwambia Trump kuwa anaamini kuwa kuwepo kwa Mkurugenzi wa mawasiliano kutatiza kazi yake katika Ikulu ya White House.

Amefananisha mabadiliko hayo kama kuwa na wapishi wengi jikoni ambao amesema wanaweza kuharibu mapishi.

Msemaji huyo wa zamani amekuwa akimtetea rais Trump na kuvishtumu vyombo vya Habari nchini humo kuwapotosha Wamarekani kuhusu uongozi wa Trump.

Trump amemshukuru Spicer kwa kazi aliyoifanya na hasa kumtetea mbele ya wanahabari nchini humo hasa kuhusu madai ya Urusi kuingilia Uchaguzi wa Marekani mwaka uliopita.

Kujiuzulu kwa Spicer kunakuja wakati huu bunge la Senate likiendelea kuchunguza madai ya Urusi kuingilia Uchaguzi huo lakini pia likiwahoji washirika wa karibu wa rais Trump akiwemo Mwanasheria Mkuu wa serikali Jeff Sessions.

Mtoto wa Trump, Donald Trump Junior anatarajiwa kuhojiwa wiki ijayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.