Pata taarifa kuu
MAREKANI-OBAMACARE-AFYA

Trump apandwa na hasira baada ya kushindwa kufuta bima ya Obamacare

Ni miaka saba chama cha Republican kikidai kufutwa na kubadilidhwa kwa sheria juu ya bima ya afya iliyopitishwa chini ya utawala wa Barack Obama mwaka 2010.

Donald Trump Julai 18, 2017 katika mkutano kuhusu afya.
Donald Trump Julai 18, 2017 katika mkutano kuhusu afya. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Donald Trump alikuwa, wakati wa kampeni zake, aliahidi, iwapo atachaguliwa, kutekeleza madai ya chama chake katika miezi ya kwanza uongozi wake. Wiki hii, matumaini ya kutimiza ahadi hiyo yamegonga mwamba.

Kama Donald Trump amesema kuwa amekata tamaa kwa kushindwa huko, hafichi kuonyesha hasira yake. Siku ya Jumatatu tena, alitangaza kwamba makubaliano kati ya wafuasi wa chama cha Republican wenye msimamo wa wastani na wale Waconservatives uko karibu kuafikiwa.

Hata kwa maseneta wawili waliopiga kura dhidi ya mradi huo wa mageuzi, mkataba huu unaweza kupitishwa. Hata hivyo, baada ya maseneta wengine wawili kupinga mageuzi hayo kuhusu bima ya Obamacare, ilikuwa pigo kubwa na aibu kwa rais Donald Trump. Bw Obama amelaumu Wademocrats ambapo maseneta 48 kutoka chama hicho walikataa kuunga mkono mageuzi hayo.

Baada ya kuona kuwa ameshindwa kwa mpango wake, rais Trump amesema hajafurahi kuona mpango wake wa mageuzi ya bima ya afya yanafeli. "Hebu tachane na mpango hiuo wa mageuzi kuhusu bima ya afya ya Obamacare, na Wademocrats watakuja kutulilia na kusema jinsi gani tunaweza kuboresha au vipi tuna mpango mpya kuhusu bima hii ya Obama care. Obamacare pigo kubwa na lni azima ibadilishwe, "alisema Donald Trump.

Kwa kupata sheria mpya, Warepublican wanaonekana kuwa hawana chaguo jingine kama ispokua kushirikiana na chama cha Democratic. Wakati huo huo, kiongozi wa wengi katika baraza la Seneti, Mitch McConnell, alitaka kupitishwa kwa mpango wa kufuta bima ya Obamacare. Hata haikuawezekana, maseneta watatu wenye msimamo wa wastani walipinga kwa sababu bila kubadilishwa, wapiga kura wa vijijini wanaowakilisha wataathirika sana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.