Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Amerika

Mpango wa kuubadilisha muswada wa Obamacare wakwama

media Tayari maseneta wawili wa Republican wamefutilia mabli muswada huo hali ambayo haingeweza kuruhusu wanachama wengine kuupinga. REUTERS/Jonathan Ernst

Baada ya rais wa Marekani Donald Trump kuahidi kuubadilisha muswada wa afya wa rais Obama kama ahadi yake wakati wa kampeni, tayari mpango huo umeenelea kuzua mgawanyiko ndani na nje ya chama cha Republican.

Maseneta wengine wawili wa chama cha Republican wanasema kuwa wanapinga mpango wa chama chao, wa kuubadilisha muswada wa afya wa Obamacare hatua iliowawacha viongozi wa Republican na uchache wa kura kufanya mabadiliko hayo.

Mgawanyiko huo unajitokeza wakati ambapo chama cha Republican kinashikilia viti 52 katika bunge la Senenti lenye wanachama 100.

Tayari maseneta wawili wa Republican wamefutilia mabli muswada huo hali ambayo haingeweza kuruhusu wanachama wengine kuupinga.

Mike Lee na Jerry Moran walitangaza hatua yao mara moja.

Maseneta hawa wote walitangaza kwamba hawawezi kuunga mkono muswada huo kama ulivyo, huku wakisema kuwa kulikuwa na matatizo mbalimbali kuhusu muswada wa Obamacare. Waliongezea kuwa ''hawawezi kuidhinisha sera mbaya''.

Hatua hiyo inaendeleza kuwatoza kodi muhimu matajiri huku ikiwaondolea mzigo watoaji huduma za bima ili kuweza kuwapunguzia malipo watu masikini wanaohitaji huduma ya afya.

Maseneta wengine wawili, Rand Paul na Susan Collins tayari walikuwa wametangaza kuupinga musawada huo.

Maseneta kutoka chama cha Democratic cha Barack Obama walikuwa wamesema kuwa hawatakubali kuubadilisha muswada huo wa Obamacare lakini wanaweza kufanya kazi kwa pamoja ili kuufanya kuwa imara.

Kufuatia tangazo hilo sasa itakuwa vigumu zaidi kwa mswada huo kuidhinishwa kama ilivyo.

Mike Lee na Jerry moran, wamesema mswada wa sasa hautoshi kufutilia mbali mpango huo wa bima ya afya maarufu Obamacare.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana