Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/05 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/05 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/05 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
  • Kesi mbili mpya za ugonjwa wa Ebola zaripotiwa DRC
Amerika

Asilimia 98 ya wapiga kura wa upinzani nchini Venezuela wapinga mabadiliko ya katiba

media Kura za maoni zikihesabiwa nchini Venezuela REUTERS/Marco Bello

Wapiga kura Milioni saba wengi wao wafuasi wa upinzani wamepiga kura nchini Venezuela, kupinga mpango wa serikali wa kuibadilisha Katiba ya nchi hiyo na kumpa mamlaka makubwa rais.

Rais Nicholas Maduro amesema kura hiyo ya maoni haina maana yoyote huku matokeo yakionesha kuwa asilimia 98 ya waliopiga kura, wamepinga katiba kufanyiwa marekebisho.

Wapiga kura pia wanataka Uchaguzi mpya kuitishwa nchini humo na kuondolewa madarakani kwa rais Maduro ambaye wapinzani wanasema ni dikteta.

Wakati uo huo, watu waliokuwa na silaha wakiwa juu ya pikipiki wamempiga risasi na kumuua mpiga kura wa upinzani nchini Venezuela wakati akiwa katika mstari wa kupiga kura ya maoni.

Imebainika kuwa mtu aliyepigwa risasi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 61 ambaye ni Nesi aliyekuwa anajiandaa kushiriki katika zoezi hilo lisilotambuliwa na serikali.

Mbali na kifo hicho, watu wengine watatu wamejeruhiwa katika shambulizi hili na wanapewa matibabu.

Msemaji wa upinzani Carlos Ocariz amesema mauaji ya mwanamke huyo yamewapa hasira na uchungu baada ya wafuasi wao 100 kupoteza maisha katika makabiliano na maafisa wa usalama kuanzia mwezi Aprili.

Kura hii ya maoni inakuja wakati huu serikali ikiandaa kura ya maoni itakayofanyika tarehe 30 mwezi huu, ili kuibadilisha katiba hiyo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana