Pata taarifa kuu
MAREKANI-HAKI

Donald Trump amtetetea mwanawe

Rais wa Marekani Donald Trump amemtetea mwanawe Donald Trump Junior, kuhusu mkutano aliofanya na wakili wa Urusi mwaka 2016 wakati wa kampeni ya urais nchini Marekani.

Donald Trump na mwanawe Don Jr. katika mkutano wa kampeni za uchaguzi Februari 1, 2016.
Donald Trump na mwanawe Don Jr. katika mkutano wa kampeni za uchaguzi Februari 1, 2016. REUTERS/Jim Bourg
Matangazo ya kibiashara

Mwana wa Trump alikutana na wakili Natalia Veselnitskaya katika jumba la Trump Tower mwezi Juni mwaka 2016.

Siku ya Jumatano Julai 11, Trump Junior alichapisha kwenye Twitter, mfululizo wa barua pepe zikionyesha kuwa alikaribisha ombi la kukutana na wakili Natalia Veselnitskaya, ambaye alikuwa na uhusiano na Urusi, ambaye alikuwa na ujumbe potovu kumhusu Hillary Clinton wakati wa kampeni za uchaguzi.

Pendekezo hilo lilipokelewa kwa furaha na mwanae Donald Trump. Kesi hii imezua mvutano katika bunge la Congress, wakati ambapo uchunguzi kuhusu kampeni kati ya Trump na Urusi unaendelea.

Gazeti la New York Times ambalo lilifichua mkutano huo wa Donald Junior na wakili wa Urusi, lilikuwa katika hatua ya kuthibitisha ukweli kuhusu uchunguzi wake.

Donald Trump Jr, mkwe wake Jared Kushner na mwenyekiti wa kampeni Paul Manafort, walikutana na wakili wa Urusi Natalia Veselnitskaya, katika jumba la Trump Tower mjini New York mwezi Juni mwaka 2016.

Wakati huo huo rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa hakufahamu lolote kuhusu mkurano wa Trump Junior na wakili Natalia Veselnitskaya.

Donald Trump Junior alikiambia kituoa cha habari cha Fox News kuwa mkutano huo haukuhusu chochote.

Hata hivyo Trump Junior, amesema kuwa hakumfahamisha babake kuhusu mkutano na wakili wa Urusi ambaye alisema kuwa angesaidia katika kampeni yake ya uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.